Jasmine Pilchard- Gosnell ( 23) , alipowasili
nyumbani kwa Paul Sant Barbara kwa ajili
ya msiba .
Paul Walker enzi za uhai wake ( kushoto) na
Jasmine Pilchard- Gosnell.
Wakati watu wakiwa na huzuni bado
kutokana na ajali iliyompata muigizaji
mwenye mvuto wa Fast & Furious Paul
Walker na kuchukua uhai wake , mapya
mengine yameibuka kwa mujibu wa mtandao
wa habari za mastaa huko majuu TMZ .
Paul mwenye miaka 40 imeelezwa amefariki
kutokana na majeraha ya moto pamoja na ya
ajali ya gari kujibamiza. Inasemekana wakati
gari aina ya Porsche waliyopanda ilipopata
ajali walikuwa hai bado lakini baada ya
kuwaka moto ndipo walipopoteza uhai maana
yake ni kwamba waliungua mpaka kufa .
Mpenzi wa siku nyingi wa Paul ( 40) , Jasmine
Pilchard-Gosnell ( 23 ) ameonekana hadharani
kwa mara ya kwanza tangu ajali hiyo itokee
alipowasili msibani Santa Barbara . Wapenzi
hawa wamedumu kwa miaka 7 tangu
walipoanza uhusino mwaka 2006 licha ya
tofauti yao kiumri wakati huyo Jasmine ana
miaka 16 na Paul 33 kwa hiyo utaona tofauti
ya umri kati yao.
Thursday, December 5, 2013
KIFO CHA PAUL WALKER MAPYA YAIBUKA , MPENZI WAKE AJITOKEZA HADHARANI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment