Nchini England mabingwa watetezi wa Ligi ya
nchi Hiyo Manchester United wameendelea na
mwanzo mbaya wa ligi hiyo baada ya hii leo
kukubali kipigo cha bao moja bila toka kwa
Newcastle United .
Bao pekee lililoacha simanzi kwa mashabiki wa
United lilifungwa na kiungo Mfaransa Yohan
Cabaye. Matokeo haya yanaiacha United kwenye
nafasi ya tisa wakiwa wameachwa na vinara wa
ligi hiyo kwa pointi 12.
Hii ni mara ya kwanza kwa United kupoteza
mechi mbili mfululizo kwenye uwanja wake wa
nyumbani tangu mwaka 2002 huku ikiwa ni mara
ya kwanza kwa Newcastle United kushinda
mchezo kwenye uwanja wa Old Trafford kwa
miaka 41.
Kocha wa Team Hiyo Ambae kwa sasa ni kama
amekalia kuti kavu amesisitiza kuwa ni lazima
asajili wachezaji wapya wakati wa majira ya
Baridi ..ili kuokoa jahazi...
Sunday, December 8, 2013
KOCHA MANCHESTER UNITED AKALIA KUTI KAVU-ASISITIZA NI LAZIMA ASAJILI WACHEZAJI WAPYA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Hahahahahaaaa
ReplyDelete