Thursday, December 12, 2013

Kocha Simba ataka dakika 180 kuimaliza Yanga


Kocha Mkuu wa Simba , Zdravok Logarusic.
Na Khadija Mngwai
KOCHA Mkuu wa Simba, Zdravok Logarusic ,
amesema anahitaji mechi mbili zaidi zikiwa ni
dakika 180 ili kuweza kukipima kikosi chake
kabla ya mechi yao ya Mtani Jembe dhidi ya
Yanga.
Mechi ya Mtani Jembe inatarajiwa kupigwa
Desemba 21 mwaka huu kwenye Uwanja wa
Taifa jijini Dar es Salaam.
Logarusic amepewa mkataba wa miezi sita
wa kuitumikia Simba baada ya kutimuliwa
kwa aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo ,
Abdallah Kibadeni .
Akizungumza na Championi Jumatano ,
Katibu Mkuu wa Simba, Evodius Mtawala ,
alisema kocha huyo tayari ameshakiona
kikosi na kusema kuwa anataka mechi mbili
kabla ya kuivaa Yanga.
“Tutacheza na KMKM lakini kocha amehitaji
mechi nyingine zaidi ambapo tutacheza mbili
kabla ya kuivaa Yanga.
“Lengo la kocha ni kuangalia uwezo wa kila
mchezaji ili aweze kuona viwango vyao na
kuweza kupanga timu. Tayari ameshawaona
kwenye mazoezi na sasa anataka awaone
jinsi wanavyocheza kwenye mechi , ” alisema
Mtawala .
Hii ina maana kuwa , kocha huyo atatumia
dakika 180 uwanjani ili kujua ni jinsi gani
timu yake inaweza kuisambaratisha Yanga.

No comments:

Post a Comment

.