Didier Kavumbagu .
Na Lucy Mgina
UONGOZI wa Yanga umesema mtu
atakayeamua hatma ya mshambuliaji wa
kimataifa wa klabu hiyo , Didier Kavumbagu ,
raia wa Burundi kubaki au kuondoka ni kocha
Ernie Brandts .
Kavumbagu aliyeifungia mabao matano
Yanga kwenye mzunguko wa kwanza wa Ligi
Kuu Bara , amebakiza mkataba wa miezi sita
tu .
Akizungumza na Championi Jumatano ,
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga,
Abdallah Bin Kleb, alisema jukumu la
kumuongezea mkataba Kavumbagu na
wachezaji wengine wanaomaliza mikataba
yao, wamelikabidhi kwa Brandts ili aamue
kila kitu .
Alisema wao kama uongozi wanamsikiliza
yeye anamtaka nani ndipo wanamuongeze
mkataba na kwamba walimpa muda
awaangalie wachezaji wa kuwaongeza
kwenye dirisha dogo .
“Suala la Kavumbagu tumemuachia kocha
kwa kuwa yeye ndiye anajua nani anamhitaji
na nani hamfai tena , siyo huyo tu na wengine
ambao wamebakiza muda mfupi kumaliza
mikataba yao, ” alisema Bin Kleb .
Thursday, December 12, 2013
Kavumbagu akabidhiwa kwa Brandts Yanga
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment