Manchester United Jumamosi lipata kipigo chake
cha pili nyumbani katika muda wa siku nne baada
ya kulazwa bao moja bila na New Castle.
Mchezaji wa New Castle Yohan Cabaye ndiye
aliipatia kilio Man U huku kwao ikiwa kicheko
baada ya kushinda Manchester United kwa mara
ya kwanza nyumbani Old Trafford tangu mwaka
1972.
Man U walikuwa na wakati mgumu kuvunja ari ya
Magpies na kukosa nafasi kadhaa za mabao
mfano Patrice Evra alipogonga lango huku mpira
ukirudi na kumgonga mkono Vurnon Anita.
Mpira wa kichwa wa Robin van Persie haukuzaa
matunda kwa Manchester United,lakini Newcastle
waliishia na kicheko baada ya kupata ushindi wao
wa kihistoria dhidi ya Man U.
Bila shaka hii inazua wasiwasi mkubwa kwa
David Moyes kwani Man U wanaendelea tu
kudidimia kwa mabao.
Man u wameshuka ngazi hasa baada ya kupata
kipigo mara mbili mfululizo tena nyumbani Old
Trafford ikiwa ni mara ya kwanza kwa hali hii
kushuhUdiwa kwa United.
Mnamo Jumatano walilazwa na Everton huku
wakiwa nyuma ya Arsenal kwa pointi 12
wakikabiliwa na tisho la kutokuwa katika msitari
wa mbele kuwania kombe la ligi ya Premier.
Ikiwa wataendelea kushindwa hivi Man U hata
huenda wasiwe katika nafasi za kwanza nne.
Saturday, December 7, 2013
Man U kipigo mfululizo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment