Sunday, December 8, 2013

MELI YA MIZIGO MV MERCI II YAZAMA KILWA MASOKO by GLOBAL


MV Merci II ikianza kuzama majini katika
gati la Kilwa Masoko .
Sehemu ya chini ya MV Merci II .
Meli hiyo ikiwa imefunikwa na maji.
MV Merci II kabla ya kuzama .
Na Abdulaziz Video, Kilwa
Meli ndogo ya mizigo ya MV MERCI II
inayomilikiwa na Semuhungu Shingiro
imezama katika bandari ya Kilwa masoko .
Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Nice
Mtega fundi mkuu wa meli hiyo anahofiwa
kufa maji baada ya kutoweka kwa zaidi ya
masaa 36 toka kuzama kwa meli hiyo .
Akiongea na Michuzi Blog , Meneja wa
Bandari ya Kilwa, Bw. Iddi Omary , alieleza
kuwa meli hiyo iliyofunga gati jana jioni
ikitokea Songosongo na kupakia tani 30 za
mchanga na tani 30 za maji ilizama majira
ya saa 6 usiku wa kuamkia leo ambapo
nahodha wake Charles Kalinga na wasaidizi
wake watatu walifanikiwa kutoka ila Nice
Mtega aliyekuwa ndani hajaonekana hadi
sasa .
Juhudi za kumtafuta na kuinua meli hiyo
zinaendelea. Sababu ya kuzama kwake bado
hazijajulikana .

1 comment:

.