Thursday, December 5, 2013

MAYA: TUMESHINDIKANA JAMANI


Stori: Brighton Masalu
MSANII wa filamu , Mayasa Mrisho ‘ Maya ’
amejikuta ‘ akiponyokwa ’ na sentensi tata
kwa kudai wasanii wengi linapokuja suala la
‘ kuponda ’ raha wamekuwa vinara hivyo
wameshindikana .
Mayasa Mrisho ‘Maya ’.
Akipiga stori na Ijumaa ndani ya viwanja vya
TCC Club Chang’ ombe jijini Dar huku
akimuegemea msanii mwenzake, Shamsa
Ford mwishoni mwa wiki iliyopita, Mayasa
alisema starehe imechukua sehemu kubwa
ya maisha ya wasanii wengi na kwamba
hakuna anayeweza kubadili staili hiyo ya
maisha.
“Ila sisi wasanii tumeshindikana kwa starehe
jamani, lakini hata hivyo kutokana na ugumu
wa kazi zetu tuna haki ya kupumzisha akili
kama hivi , acha tule raha bwana, ” alisema
Maya huku akigonganisha ‘ chiaz ’ na wasanii
wenzake .

1 comment:

.