DUNIA ipo kimya wakati maandalizi ya
kuupumzisha kaburini mwili wa aliyekuwa
rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini,
Nelson Mandela yakiendelea katika miji ya
Johannesburg, Pretoria na kijijini Qunu , Mkoa
wa Mthatha jimboni Eastern Cape atakozikwa
kijijini atakakozikwa .
UKIMYA WATANDA KWENYE TELEVISHENI
Ukimya uliendelea kutawala juzi na jana
katika miji mbalimbali duniani , watu
walikusanyika kwenye televisheni za wazi
kufuatilia zoezi la kuuaga mwili huo
zilizofanyika katika Jengo la Umoja jijini
Pretoria.
Maelfu ya waombolezaji walionesha kuguswa
kwa kiasi kikubwa na msiba huo unaotajwa
kushika rekondi tangu kuwepo kwa
ulimwengu kuwahi kutazamwa na watu wengi
zaidi kuliko mingine yote iliyowahi kutokea.
Mazishi ya aliyekuwa Kiongozi Mkuu wa
Kanisa la Romani Katoliki Duniani, Papa John
Paul wa II unatajwa kushika rekodi ya
kwanza hadi Desemba 5 mwaka huu
alipokufa Mandela.
PICHA ZA TELEVISHENI ZATAWALIWA NA
VIDEO ZA MANDELA
Vituo vingi vya televisheni sehemu
mbalimbali ulimwenguni, licha ya kuonesha
tukio hilo la kuaga mwili , pia viliweka video
ya matukio mbalimbali yaliyowahi kufanywa
na kiongozi huyo anayetajwa kama
mwanamapinduzi wa kweli , mpigania haki na
mwanaharakati aliyeheshimika kuliko
mwingine katika karne ya 21.
Baadhi ya matukio hayo ni pamoja na jinsi
alivyoshiriki shughuli mbalimbali duniani
ikiwa ni pamoja na kupiga picha na
wanamichezo , wasanii wengi maarufu ,
ambao pia walionesha kufurahishwa naye
kila alipokutana nao .
SERIKALI SAUZI YASAMBAZA SETI YA
TELEVISHENI NCHI NZIMA
Serikali ya Afrika Kusini imesambaza seti ya
televisheni zipatazo 90 nchi nzima na
kuwekwa katika maeneo mengi ya wazi kwa
lengo la kuwawezesha mamilioni ya
wananchi wake kuangalia shughuli za
kumuaga kiongozi huyo zinavyokwenda.
KIJIJINI QUNU KAMA MJINI
Katika Kijiji cha Qunu alichokulia hayati
Mandela, maandalizi ya kaburi atakalozikwa
yapo tayari huku kijiji hicho kikijaa watu na
kuwa na maisha kama mjini.
Magari ya kila aina yanaingia na kutoka ,
watu wasiofanana na maisha ya kijijini
wanapatikana kwa sasa , wengi wao wakiwa
wageni , wakiwemo wa vyombo vya habari,
wanaingia na bidhaa zao, hususan chakula .
NDEGE YA KIJESHI KUMPELEKA MANDELA
KIJIJINI KWAKE
Serikali ya nchi hiyo imetamka kuwa , mwili
wa hayati Mandela utapelekwa kijijini Qunu
kwa ndege ya jeshi la nchi hiyo , tayari kwa
mazishi yake Jumapili ya Deseamba 15 .
WAZEE WA KIMILA WATOA MSIMAMO
KUHUSU MAZISHI
Taarifa kutoka kijijini hapo zinasema kuwa
jamii ya Kabila la AbaThembu ( ndivyo
inavyaondikwa) , imetaka kukabidhiwa
shughuli za mazishi hayo ili shujaa huyo
aweze kuzikwa kwa mujibu wa mila za kabila
lake.
Kiongozi wa jamii ya Xhosa ( lugha ya Waaba
Thembu) , Nokuzola Mndende alisema kuwa
endapo serikali itapuuza matakwa yao ipo
hatari ya Mandela kutopokelewa na miungu
hivyo roho yake kurejea duniani na
kuisumbua familia yake.
“Zitakuwa ni mila na desturi za jadi, serikali
inapaswa kutupa nafasi na isituingilie .
Ng’ ombe dume ( fahali) atachinjwa kwa ajili
ya kumsindikiza marehemu kaburini , ” alisema
kiongozi huyo bila kupindisha maneno
kinywani.
Aliongeza: “Katika utaratibu huu wa mazishi
ya kimila ni familia ya Mandela pekee ndiyo
watakaohusika kumwandalia safari njema
Madiba .”
Kwa mujibu wa desturi za mazishi za kabila
hilo, mtu aliyefariki dunia endapo alikuwa
kiongozi , hupewa heshima ya kuchinjiwa
ng’ ombe dume ili amsindikize ambapo damu
yake hunyunyiziwa juu ya kaburi .
TARATIBU ZA MAZISHI ZA KIKABILA
Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali , zipo
taratibu maalum ambazo ni lazima zifuatwe
wakati wa mazishi ya mtu wa kabila moja na
mzee Mandela .
Baada ya mtu kufariki dunia , ni jukumu la
wanafamilia ya marehemu kutangaza msiba
huo kwa ndugu na jamaa ili waweze
kukutana na kusaidiana wakati wa mazishi .
Kabla ya ujio wa vyumba vya kisasa vya
kuhifadhia maiti ( mochwari ) , Waaba Thembu
walikuwa wakimzika mtu siku hiyohiyo kwa
kuhofia mwili wake kuharibika .
Kabla ya kufanyika kwa mazishi , taratibu
zinasema vyombo vyote vilivyomo ndani ya
nyumba hutolewa nje na wanawake
wanaohusiana na marehemu ni lazima
wafanye usafi katika nyumba aliyokuwa
akiishi.
Katika siku za nyuma , kuta za kibanda
kikubwa kilichokuwa kikitumiwa na marehemu
kulala kilikandikwa udongo , lakini hivi sasa
nyumba kubwa kwa kawaida husafishwa na
kupakwa rangi upya.
Baada ya usafi huo , mkeka wa kiasili
huwekwa katika chumba kikubwa cha kulala
ambako mjane wa marehemu hutakiwa
kukalia mkeka huo unaowekwa chini ya
dirisha.
Uchaguzi wa ng’ ombe mnono wa kiume
hutegemea na umuhimu wa marehemu na
wanaume ndiyo wanaopika nyama hiyo katika
vyungu vya kikabila ikichemshwa bila
kuwekwa kiungo chochote.
Tukio hili huitwa Umkhapho inayodaiwa
kuwa ni mizimu ya kumsindikiza mtu
aliyefariki dunia .
Friday, December 13, 2013
MAZISHI YA MANDELA , DUNIA KIMYA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment