Stori: Dustan Shekidele , Morogoro
KUCHA za Shetani zimeugusa uchumba wa
muda mrefu kati ya msanii Selemani Msindi
‘ Afande Sele ’ na Asha Shiengo ‘ Mama
Tunda’ ambapo inadaiwa sasa kila mmoja
yuko na ‘ hamsini ’ zake, Ijumaa
linaibumburua .
Picha ya familia: Kutoka kulia ni Asha
Shiengo ‘Mama Tunda ’, Selemani Msindi
‘Afande Sele’, Asantesana Selemani
na Tunda Selemani.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, kutoelewana
kwao kunachangiwa na kucheleweshwa kwa
ndoa baina yao pamoja na mambo mengine
ambayo hakuwa tayari kuyaanika .
“Kwa kifupi mapenzi sasa hivi kati ya Afande
na Mama Tunda ni ‘ vululuvululu ’ , kila mmoja
yuko kivyake .
“Chanzo kikubwa ni kucheleweshwa kwa
ndoa ambapo Afande anaonekana kupotezea
suala la kuoana , ” kilisema chanzo hicho kwa
sharti la kutotajwa jina lake gazetini.
Mwandishi wetu alipomtafuta Afande Sele
kuweka wazi juu ya tuhuma hizo , kwa sauti
ya upole kabisa alikiri kutokuwepo
maelewano baina yake na mzazi mwenziye
huyo huku akishindwa kubainisha haswa
chanzo cha kutengana kwao .
“Ni kweli , kwa sasa siko na Mama Tunda,
mimi niko Morogoro na yeye yuko Dar , ”
alisema msanii huyo bila ufafanuzi wa ziada.
Hata hivyo Mama Tunda alipotafutwa kwa
njia ya simu, alissema chanzo cha mambo
yote ni kutovalishwa pete ya ndoa .
“Chanzo ni hicho tu , nimechoka kukaa
kwenye uchumba kwa muda mrefu ni miaka
15 sasa , hadi Tunda amefikisha miaka 13 , si
ni ajabu hiyo na sasa tuna mtoto wa pili
ambaye ana miaka 2 bado ni wachumba tu ,
nimechoka,” alisema Mama Tunda na kisha
kukata simu.
Wawili hao wamejaliwa watoto wawili, Tunda
Selemani ( 13) na Asantesana Selemani ( 2) .
Friday, December 13, 2013
PENZI LA AFANDE SELE , MAMA TUNDA VULULUVULULU
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Shuguli
ReplyDelete