Tuesday, December 10, 2013

Mbeya City : Tunamaliza ubabe wa Simba, Yanga msimu huu


TIMU ya Mbeya City imepanga kufanya
maajabu katika msimu huu wa Ligi Kuu
Tanzania Bara kwa kuhakikisha inachukua
ubingwa huo unaotetewa na Yanga.
Mbeya City imepanda daraja msimu huu wa
ligi na kufanikiwa kuleta changamoto kubwa
kwa klabu kongwe za Simba, Yanga na Azam
FC.
Timu hiyo imefanikiwa kumaliza mzunguko
wa kwanza ikiwa katika nafasi ya tatu, jambo
ambalo limewashangaza wengi .
Akizungumza na Championi Jumatano , Ofisa
Habari wa Mbeya City , Fred Jackson , alisema
watahakikisha wanapambana na timu za
Simba na Yanga ambazo zimezoeleka
kuchukua ubingwa kila msimu .
Jackson alisema wamepanga kufanya
maajabu kwa kuwashitua Simba na Yanga,
wanaamini watafanikiwa kutokana na ubora
wa kikosi chao.
Aliongeza kuwa , mazoezi rasmi
yamekwishaanza kwa ajili ya maandalizi ya
ligi kuu na Kombe la Mapinduzi ambalo
linaanza mapema mwanzoni mwa mwezi ujao
visiwani Zanzibar.
“Ninaamini timu yetu itachukua ubingwa
msimu huu kwa mara ya kwanza ikiwa ni
msimu mmoja tangu tumepanda daraja
kucheza ligi kuu.
“Hayo ndiyo malengo yetu tuliyojiwekea, siyo
vinginevyo, tutahakikisha tunavunja mwiko
wa Simba na Yanga kwa zenyewe kuchukua
ubingwa pekee kila msimu .
“Hatuogopi timu yoyote, tunaangalia mipango
yetu na malengo yetu tuliyojiwekea tokea
mwanzoni, japo wengi watashangaa kwa nini
tuzungumzie ubingwa wakati bado ni
mapema .
“Lakini bado tumepata heshima kubwa kuwa
na mwaliko Zanzibar kwenye Kombe la
Mapinduzi, ni lazima tujiandae vizuri ili
kuendeleza heshima ya timu yetu tukienda
kule na kufanya vizuri, ” alisema Jackson .

No comments:

Post a Comment

.