Na Nicodemus Jonas
TIMU ya Coastal Union ya Tanga,
imefanikiwa kumnasa mshambuliaji raia wa
DR Congo , Eyale Abrave , akitokea Klabu ya
Lupopo ya nchini humo .Nyota huyo
anatarajiwa kusaini kesho ( Alhamisi )
mkataba wa miaka miwili .
Akizungumza na Championi Jumatano ,
meneja wa mchezaji huyo, Paul Lungele ,
alisema tayari kila kitu wamemalizana na
ametumiwa tiketi ya ndege akitokea kwao DR
Congo.
“Tumemalizana na timu yenyewe , pia
wamemtumia tiketi kwa ajili ya kuhakikisha
Alhamisi anafika Tanga ili kusaini na atapewa
mkataba wa miaka miwili ,” alisema .
Aidha , alipoulizwa Ofisa Habari wa Coastal
Union, Hafidhi Kido , alisema hawezi
kukanusha wala kukubali kumalizana na
nyota huyo kwani ni kweli wamekuwa kwenye
mazungumzo naye siku za hivi karibuni .
“Siwezi kuthibitisha wala kukataa , ninachojua
ni kweli tumekuwa na mawasiliano naye na
taarifa ya mwisho ni kwamba kufikia Ijumaa
wiki hii tungekuwa tumemalizana naye , ”
alisema Kido .
Ujio wa Abrave unaongeza hofu kwa straika
wa Uganda , Yayo Lutimba , ambaye amekuwa
akihusishwa na taarifa za kutemwa katika
usajili wa dirisha dogo mwezi ujao.
Tuesday, December 10, 2013
Coastal yamnasa straika kutoka Lupopo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment