Sunday, December 8, 2013

MBUNGE AMSHAURI RAIS KIKWETE KUMG'OA WAZIRI MKUU PINDA ADAI HAWAJIBIKI NI MPOLE MNO


Dodoma. Rais Jakaya Kikwete, ameshauriwa
kumng’oa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ikielezwa
sababu kuwa ndiye kikwazo katika utendaji wa
Serikali na kwamba akiachwa ataipeleka pabaya
Serikali na CCM
Kikwete pia ameshauriwa kumfukuza kazi Waziri
wa Tamisemi, Hawa Ghasia, kwa kushindwa
kukabiliana na matatizo ya ubadhirifu katika
halmashauri nchini.
“Kama (Rais) unaitakia mema nchi na CCM
kuchukua hatua za kuwafukuza kazi Pinda na
Waziri Ghasia,” alisema Mbunge wa Mwibara,
Khangi Lugola (CCM), juzi alipochangia taarifa
za Kamati za Bunge kuhusu hesabu za Serikali
kwa mwaka wa fedha ulioishia Juni 30 mwaka
jana.
“Kwa nini Watanzania wafe kwa kunyimwa
misaada na wafadhili kwa sababu ya mtu mmoja
tu Pinda, kwa ajili ya Ghasia ameiendesha
Tamisemi kama Saccos ama Vikoba?” alihoji.
“Mchawi wetu ... ni Waziri Mkuu Mizengo Pinda
amekuwa mpole mno hawajibiki,” alisema Mh.
Lugola na kuongeza, “Kuanzia jana (juzi) Waziri
Mkuu anahudhuria mahafali.”
Wakati Lugola akizungumza mawaziri
waliokuwepo bungeni ni wanne, manaibu
mawaziri wawiliwawili, wakati mawaziri wote
53.

1 comment:

.