Thursday, December 5, 2013

Mjomba’ke Rais Obama ashinda kesi na kuruhusiwa kuishi kihalali Marekani


MJOMBA wa
Rais Barack
Obama wa
Amerika, Bw
Onyango
'Omar’ Obama,
ameruhusiwa
aendelee kuishi
nchini humo
na Mahakama
ya Uhamiaji
kufuatia kesi
ya kufukuzwa
kwake
iliyofanyika
Jumanne.
Jaji wa Uhamiaji Amerika, Bw Leonard Shapiro
alimruhusu Bw Onyango mwenye umri wa miaka
69 aendelee kuishi nchini humo na kumzuia
kuhamsishwa Kenya, kwa kusema ametimiza
mahitaji ya kukabidhiwa kibali cha 'Green Card’.
Kwenye uamuzi wake, Jaji huyo alisema anaamini
Bw Onyango ni muungwana, jirani mwema na
hulipa ushuru inavyohitajika.
Jaji Shapiro alisema anatumia sheria inayoruhusu
wahamiaji wasiotambulika na taifa lolote wawe
wakazi wa kudumu ikiwa waliwasili Amerika kabla
1972, wakaendelea kuishi huko na wenye tabia
njema.
Bw Onyango amekuwa akiishi Amerika kwa miaka
50 sasa, kwani aliwasili huko 1963.
Alikuwa ameamrisha kuhama 1992 ingawa
alikaidi agizo hilo na akabaki nchini humo.
Haikujulikana alikuwa bado yuo Amerika hadi
alipokamatwa kwa kuendesha gari akiwa
mlevi 2011, mjini Framingham, magharibi mwa
Boston.
Baada ya kukamatwa kwake, amri ya kuhamishwa
kwake iliyokuwa imetolewa awali ilianza
kujadiliwa upya.
Alifikishwa mahakamani alipokamatwa
akiendesha gari akiwa mlevi ingawa Jaji
aliyesimamia kesi hiyo aliiendeleza kwa mwaka
mmoja bila kutoa hukumu, na kusema kesi hiyo
ingeondolewa iwapo Bw Onyango hatakamatwa
tena wakati huo.
Alipoulizwa na Mahakama ya Uhamiaji ikiwa
alikuwa na familia Amerika, alisema, “Nina mpwa.
Barack Obama, ndiye Rais wa Amerika.”
Bw Onyango sasa ameruhusiwa kuomba kuwa
mkazi wa kudumu, ambayo itampatia haki ya
kufanya kazi kihalali Amerika na kusafiri nje ya
nchi hiyo.
Mnamo Mei 2010, dadake Zeituni Onyango
aliruhusiwa kuishi Amerika baada ya kudai kwa
kuwa ni Mjaluo, maisha yake yangekuwa hatarini
iwapo angehamishwa kurudi Kenya.
Bi Onyango aliwasili Amerika 2000, na alijaribu
kuomba aruhusiwe kuishi Amerika 2004 ingawa
aliamrishwa kuhama na Jaji Shapiro.
Hata hivyo, Bi Onyango hakuhama na badala yake
aliishi katika nyumba zinazomilikiwa na Serikali
ambazo kwa kawaida hutumiwa na wakazi halali
wa Amerika na wananchi wenye mapato ya chini,
ambao huwa hawaitajiki kuzilipia au hulipa kiasi
kidogo cha pesa.
Punde baada ya ombi lake la pili kuruhusiwa,
alinukuliwa kwenye vyombo vya habari akisema
Amerika ilikuwa na haki ya kumruhusu awe raia
kwa kuwa alikuwa mhamiaji.
“Ikiwa nilikuja kama mhamiaji, mko na jukumu la
kunifanya niwe raia,” aliambia kituo cha
televisheni cha WBZ kilicho Boston.
Ingawa Zeituni Onyango na kakake wanaweza
kuishi Amerika kihalali na kusafiri nje ya nchi
wanavyotaka, Bi Onyango hawezi kusafiri
kuelekea Kenya kwa kuwa alikabidhiwa uraia kwa
misingi ya kuwa ilikuwa hatari kwake kuwepo
Kenya.
-- via SwahiliHub
-- English version: NBCNews.com

No comments:

Post a Comment

.