Sunday, December 15, 2013

MKE WA MTU ABAKWA , ANYONGWA


Stori: Mayasa Mariwata na Chande Abdallah
JAMANI jamani ! Dunia imefika pabaya zaidi ,
Mungu asaidie . Mwanamke mkazi wa
Chalinze, Mkoa wa Pwani , Moshi Rashid ( 43 )
amefanyiwa unyama uliopitiliza na watu
wasiojulikana baada ya kumbaka na
kumnyonga , inauma sana kwa kweli !
Mwanamke mkazi wa Chalinze, Mkoa wa
Pwani , Moshi Rashid ( 43) amefanyiwa
unyama uliopitiliza na watu wasiojulikana
baada ya kumbaka na kumnyonga.
Tukio hilo la kutisha lilijiri usiku wa Desemba
7, mwaka huu Chalinze Kwamwarabu ambapo
mwanamke huyo alikwenda kujumuika na
ndugu na majirani katika mkesha wa ngoma
ya kuwatoa wari siku ya Jumapili .
Eneo la tukio Chalinze Kwamwarabu .
Mkasa huu unasimuliwa kwa majonzi mazito
na mdogo wa marehemu ambaye alikuwa
mshehereshaji wa shughuli hiyo ‘ MC ’ ,
Siwema Rashid .
Alisema: “Mpaka sasa tunashindwa kuelewa
kilichotokea maana siku ya tukio tulikuwa
naye kwenye ngoma usiku . Alikuwa
mchangamfu sana, aliifanya shughuli
ipendeze.
“Ilipofika saa nane usiku baadhi ya watu
walianza kulala , sasa sijui yeye ilikuwaje
mpaka hali hiyo ikamfika maana hao watu
walichomfanyia wametuachia historia kubwa
sana.
“Walimbaka wakaona haitoshi wakamwingiza
chupa ya soda sehemu ya siri ya mbele
halafu wakamwingiza chupa ya bia sehemu
ya siri ya nyuma .
“Ili kuzidi kutimiza unyama wao , waliondoka
na kumwacha kama alivyozaliwa , inauma
sana halafu matukio ya hivyo yamekithiri
sana.”
Aliongeza: “Marehemu ametuachia jukumu la
malezi kwa watoto wake wawili, Sikudhani
Juma ( 18 ) na Ally Juma ( 12) . ”
Naye mtoto mkubwa wa marehemu ,
Sikudhani akisimulia kifo cha mama yake,
alisema : “Nasikitika sikuweza kuuona mwili
wa mama hata pale watu walipojazana na
kumshangaa .
“Hata polisi na mganga mkuu wa mkoa
walipofika kumchomoa zile chupa sikutaka
kusogea kabisa , naamini Mungu
atawaonesha jambo hao watu hapahapa
duniani. ”
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani , Yurichi
Mtei akizungumzia ukatili huo alisema :
“Taarifa za tukio hilo bado hazijafika kwangu
kutokana na majukumu mengine ya kikazi,
isipokuwa nalifanyia kazi kuhakikisha
watuhumiwa wanakamatwa . ”
Tukio hilo lilifunguliwa jalada kwenye Kituo
cha Polisi Chalinze kwa namba CH/
RB /3767 /2013 MAUAJI .
Mpaka kifo chake , mwanamke huyo alikuwa
akiishi na mwanaume mmoja ( jina
halikupatikana mara moja lakini si aliyezaa
naye watoto hao wawili) . Alizikwa Jumapili
iliyofuata , Chalinze .
Mungu ailaze pema peponi roho yake. Amina.

1 comment:

.