Stori: JOSEPH NGILISHO , Arusha
AMA kweli dunia sasa inaserereka! Katika
hali ya kusikitisha , baba mzazi mwenye
familia ya watoto watatu , mkazi wa Kambi
ya Fisi jijini hapa , anashikiliwa na polisi kwa
tuhuma za kumbaka binti yake wa kumzaa
hadi mtoto akafungua kinywa na kusema :
“Nimechoka kubakwa na baba . ”
Mtoto aliyebakwa na baba yake mzazi .
Tukio hilo lililobumburuka hivi karibuni
limewaacha watu vinywa wazi kwa sababu
mtoto huyo ana umri wa miaka minane na
kwamba alianza kufanyiwa ukatili huo mwaka
jana akiwa na umri wa miaka saba alipokuwa
darasa la pili katika shule moja ya msingi
jijini hapa ( jina tunalo) .
AFUMWA LAIVU !
Inadaiwa kwamba mtuhumiwa huyo
aliyetajwa kwa jina moja la Pelejai ( 34)
ambaye ni mfanyabiashara wa mkaa,
amemwingilia mwanaye huyo kwa mwaka
mmoja .
Taarifa zinasema , mwaka jana baba huyo
aliwahi kufumwa laivu na mkewe akimtendea
ubaya huo binti yake huyo.
Hata hivyo , inasemekana kuwa baada ya
kunaswa chumbani kwake na mtoto ,
alimuomba msamaha mkewe ambaye
alimsamehe kwa sharti la kutorudia tena
kufanya tendo hilo la aibu na jambo hilo
likawa siri kati yao.
Akizungumza kwa uchungu na gazeti hili
akiwa katika Hospitali ya Mkoa ya Mount
Meru anakopatiwa matibabu , mtoto huyo
alisema chanzo cha baba yake kumbaka ni
baada ya mzazi huyo kugombana na mama
yake ambaye aliondoka nyumbani na kwenda
kwao .
Waziri wa
Maendeleo ya Jamii , Jinsia na Watoto,
Sophia Simba .
MARA YA KWANZA
Alisema mara ya kwanza kuingiliwa na baba
yake alisikia maumivu makali mno huku
akitokwa na damu nyingi .
Alieleza kuwa alijaribu kulia na kupiga kelele
usiku huo lakini baba yake alimziba mdomo
ili asitoe sauti .
Alisema alipomaliza kumfanyia ‘ unyambilisi ’
huo alimtishia kuwa endapo atasema popote ,
yeye atakamatwa na kufungwa na wao
watabaki bila baba , hivyo watateseka kwa
njaa.
Baada ya muda mtoto huyo alieleza kwamba
baba yake huyo aliendelea kumwingilia mara
kwa mara wakati kaka yake mkubwa
wanayeishi naye akishindwa kusema baada
ya kupewa fedha na baba yake.
MY GOD! KITANDA KIMOJA !
Alisimulia zaidi mtoto huyo alisema kwamba
alikuwa akilala na baba yake kitanda kimoja
kila siku kama mke na mume katika kipindi
ambacho mama yake alipokwenda kijijini
kwao Nduruma wilayani Arumeru kujifungua
na kukaa kwa zaidi ya miezi mitatu .
“Ukweli nilichoka kubakwa na baba yangu
lakini chanzo cha yote ni mama kutokuwepo
nyumbani ,” alisema mwanafunzi huyo.
Kwa upande wake , mama mzazi wa mtoto
huyo alisema kuwa aligundua tukio la
kubakwa kwa mwanaye tangu Machi mwaka
huu na baada ya tukio hilo mumewe
alimwomba tena msamaha kwa mara
nyingine na yeye kumsamehe.
Mama huyo alisema kwamba alilazimika
kwenda nyumbani kwao baada ya ujauzito
aliokuwa nao kuwa mkubwa .
Alisema baada ya kujifungua aliendelea kuishi
huko hadi Novemba 28 , mwaka huu
alipolazimika kurejea na kichanga chake
baada ya kupata taarifa za kupotea kwa
mtoto wake huyo anayedaiwa kubakwa na
baba yake.
Alisema aliporejea nyumbani kwake Kambi ya
Fisi alimuuliza mtoto wake mkubwa iwapo
baba yake alirudia tabia ya kumbaka
mwanaye lakini mtoto huyo hakusema
chochote.
Akiwa anatafakari sehemu alipokuwa
mwanaye ndipo alipopata taarifa kwamba
alikuwa kituo cha polisi alikopelekwa na
walimu wake baada ya watoto wenzake
kutoa taarifa kwa walimu kuwa mwanafunzi
mwenzao amekuwa akibakwa na baba yake
mzazi .
SHULENI
Mmoja wa walimu katika shule hiyo
alithibitisha kubakwa kwa mwanafunzi huyo
baada ya kumhoji na kumkagua na kugundua
kwamba ameharibika sehemu nyeti na kuwa
kama za mtu mzima .
IGP - Said Mwema .
HOSPITALINI
Mama wa mtoto huyo akisaidiwa na walimu
walitoa taarifa kituo cha polisi na kupatiwa
hati ya matibabu ( PF - 3) na kumpeleka
Hospitali ya Mount Meru .
Mwalimu wa shule hiyo alisema baada ya
vipimo, daktari alithibitsha kwamba mtoto
huyo alibakwa na kuharibiwa sehemu zake za
siri.
Baada ya taarifa hizo kulifikia jeshi la polisi ,
vijana wa Inspekta Said Mwema walimtia
mbaroni mtuhumiwa huyo na kumfungulia
kesi ya ubakaji kwa hati ya mashtaka AR /
RB/16064 /2013 -
UBAKAJI
Uchunguzi wa tukio hilo ukikamilika,
mtuhumiwa atafikishwa mahakamani ili
sheria ichukue mkondo wake.
INAUMA SANA !
Hivi karibuni kumeibuka vitendo vingi vya
ubakaji na unyanyasaji kwa watoto, hivyo
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na
Watoto, Sophia Simba na taasisi nyingine za
utetezi wanaombwa kuingilia kati ili
kuwanusuru watoto na ukatili huo .
Saturday, December 7, 2013
MTOTO ALIA NA KUSEMA: NIMECHOKA KUBAKWA NA BABA !
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Daah wanaume wanyama sana
ReplyDelete