Saturday, December 7, 2013

FAMILIA YA MWINYI YAZUA TAFRANI


FAMILIA ya Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili,
Alhaji Ali Hassan Mwinyi juzikati ilizua tafrani
mtaani kufuatia mzozo mkubwa wa nyumba
kati ya mjukuu wa Mzee Mwinyi , Abdi
Hassan Mwinyi na anayedai ni mmiliki wa
kurithi, Edward Francis Bogwe .
Hii ndo nyumba yenyewe juzikati ilizua
tafrani mtaani kufuatia mzozo mkubwa wa
nyumba kati ya mjukuu wa Mzee Mwinyi,
Abdi Hassan Mwinyi na anayedai ni mmiliki
wa kurithi, Edward Francis Bogwe.
Tukio hilo lilijiri mwishoni mwa wiki iliyopita,
Mwananyamala - Komakoma, Dar ambapo
mtoto wa rais mstaafu huyo aitwaye Abas
Mwinyi aliongoza sekeseke mtaani .
Mtoto wa Mwinyi ( wa pili kutoka kushoto) ,
Abas akiwa nyumbani hapo .
Ishu ilikuwa hivi ; miezi kadhaa iliyopita ,
Edward alimfikisha Mahakama ya Ardhi chini
ya Jaji Kombolwa , Abdi akimtaka ahame
kwenye nyumba hiyo ambayo ni mali ya
familia, aliachiwa na marehemu baba yake,
Francis Bogwe.
Baada ya kusikiliza utetezi wa pande zote
mbili, mahakama ikaamuru Abdi ahame
kwenye nyumba hiyo kwa vile ni mali ya
Francis.
Francis akiongozana na madalali alikwenda
kumtoa Abdi na vitu vyake , ikiwemo familia
na kupiga kufuli milango muhimu ya kuingilia
ndani na kuondoka nyumba ikiwa tupu.
Lakini siku mbili mbele , Abas akiwa na ndugu
zake wengine pamoja na askari kibao,
sambamba na huyo Abdi alifika akiwa na
karatasi mkononi yenye maagizo kutoka
Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi ikidai
kuwa , Abdi aendelee kuishi ndani ya nyumba
hiyo hadi keshi ya msingi iliyofunguliwa na
Abas ya kupinga kuhamishwa kwa Abdi
itakaposikilizwa.
Kesi hiyo ilisikilizwa Desemba 2 , mwaka huu
kwenye mahakama hiyo jijini Dar .
Baada ya kufika kwenye geti la nyumba hiyo
na kukuta watoto wa familia ya Bogwe,
akiwemo dada wa Francis aitwaye Josephine
Bogwe, Abas alisema : “Shida yetu fungueni
mlango tuingie ndani hii ni nyumba yetu
mambo mengine tutajuana
mahakamani.” ( huku akionesha hati kutoka
Mahakama ya Ardhi) .
Baada ya kauli hiyo ndipo tafrani ilipoibuka
ambapo Josephine alitoa makaratasi
yanayoonesha kuwa , nyumba hiyo ni haki
yao kama familia .
Josephine alimtaka Abas na ndugu zake
waoneshe vielelezo vyao vinavyoonesha kuwa
nyumba hiyo ni yao.
“Hapa hadi kieleweke mnataka kutudhulumu
haki yetu , haiwezekani mahakama itupatie
haki nyinyi mnakuja na maaskari kuamuru
nyumba ifunguliwe ili muingie ndani, ” alisema
Josephine .
Hata hivyo , katika kesi iliyofunguliwa na Abas
kwenye Mahakama Ardhi, Jaji Mziray alisema
Abdi si mmiliki halali wa nyumba hiyo kwa
kuwa hana nyaraka zinazoonesha aliuziwa
nyumba hiyo na marehemu Francis .
Kwa upande wa Edward , Jaji Mziray alisema
kwamba hakutakiwa kumuhamisha Abdi mara
ya kwanza bila kupata hati ya hukumu
akatakiwa kushughulikia hati hiyo kwanza .

No comments:

Post a Comment

.