Jeshi la polisi mkoani Arusha limemshikilia na
kisha kumwachia “chapchap” mtoto wa
mwenyekiti wa CCM wilaya ya Siha mkoani
Kilimanjaro na mfanyabiashara maarufu
nchini,Oscar Themi kwa kosa la kumpiga risasi
ya kichwa mhudumu wa bar ya Empire iliyopo
eneo la Shoprite jijini Arusha.
Mtuhumiwa huyo ,Dereck Themi alishikiliwa na
polisi mwishoni mwa wiki iliyopita mara baada
ya kutofautiana na mhudumu huyo wakati
alipompatia bili ya vinywaji aliyokuwa akitumia
ndani ya bar hiyo kabla ya kumtandika risasi.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa mashuhuda
wa tukio hilo walidai kuwa mnamo novemba 29
mwaka huu majira ya saa 7.30 usiku mtoto huyo
wa kigogo alimfyatulia risasi mhudumu huyo
aliyetambulika kwa jina la Witness Erasto wakati
alipompatia bili ya vinywaji.
Mashuhuda walidai kuwa kulitokea na hali ya
tofauti kati yao ambapo Themi alikubali kulipa
bili hiyo ambapo alichukua fedha na kisha
kumwekea katika matiti yake na ghafla
kuchomoa bastola yake na kisha kumtandika
eneo la kichwa.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo
walisema kuwa mara baada ya tukio hilo ndipo
mtuhumiwa alijaribu kukimbia nje ya bar hiyo
kuelekea usawa wa eneo la maegesho la magari
lakini kabla hajafika alifyatua risasi nyingine
zaidi ya tano hali iliyopelekea tafrani katika eneo
la Shoprite.
Hatahivyo,taarifa hizo zimedai kuwa askari
mmoja aliyekuwa akilinda benki ya Exim iliyopo
ndani ya eneo hilo la Shoprite alimvizia kimafia
na kisha kumnyang”anya bastola hiyo
mtuhumiwa kabla ya kuwataarifu polisi waliofika
eneo hilo na kisha kumfikisha katika kituo kikuu
cha polisi cha kati.
Mtuhumiwa huyo alifikishwa katika kituo hicho
na kisha kukabidhi bastoa hiyo pamoja na
maganda matano ya risasi ambapo baada ya
muda aliwasili mdogo wake aliyetambulika kwa
jina la Bernad Themi aliyechukua mali zake na
fedha.
Akihojiwa na gazeti hili majeruhi wa tukio hilo
Erasto alisema kuwa hawezi kuongea chochote
kwa kuwa hali yake ni sio nzuri lakini
alipotafutwa mmiliki wa bar hiyo,Tumaini Ulomi
alikiri kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa
tayari wameshafungua mashtaka mbalimbali
ikiwemo hasara aliyoipata siku ya tukio.
Mmiliki huyo alisema kuwa mara baada ya milio
ya risasi kuanza kurindima ndani ya bar yake
wateja mbalimbali wakiwemo watalii
walitokomea kusikojulikana bila kulipa hali
ambayo imemtia hasara kubwa.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoani
Arusha,Liberatus Sabas alikiri kutokea kwa tukio
hilo na kusema kwa kifupi kwamba bado
wanafanya uchunguzi wa kina kabla ya
kulifikisha suala hilo mahakamani.
Credit :libeneke la kaskazini
Thursday, December 5, 2013
MTOTO WA KIGOGO MKOANI ARUSHA AMPIGA MFANYAKAZI WA BAR RISASI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment