Sunday, December 8, 2013

Mzungu rasmi atema sita Simba


Kocha Mkuu wa Simba , Zdravok Logarusic.
Na Khatimu Naheka
KOCHA Mkuu wa Simba, Zdravok Logarusic ,
amemaliza kazi ya kwanza katika kusaka
nyota atakaoanza nao safari ya ubingwa
katika timu hiyo , ambapo tayari amefyeka
nyota sita wa kikosi hicho.
Akizungumza na Championi Jumatatu,
Logarusic , maarufu kwa jina na Loga ,
amesema kazi hiyo ya kufyeka nyota hao
aliyoifanya na msaidizi wake Seleman Matola ,
ina lengo moja kubwa katika kusaka kikosi
sahihi cha timu hiyo kitakachoweza
kurudisha heshima ya klabu hiyo kwa kushika
nafasi mbili za juu, likiwemo lengo la
kuchukua ubingwa .
Loga, raia wa Croatia, amesema nyota sita
ambao amewatema katika kikosi hicho ni
kipa Andrew Ntalla , Sino Agustino, Marceil
Kapama, Twaha Shekuhe, Rashid Ismail na
Adeyum Seif . Amewakabidhi kwa uongozi wa
timu hiyo ambao utaangalia pa kuwapeleka.
“Nilikwambia awali kuwa sitaki kuwa na
wachezaji wengi sana katika timu yangu,
nataka kuona Simba inarudisha heshima
yake, haina maana timu inakuwa na wachzaji
36 na baadaye inashika nafasi ya nne kwenye
ligi , ” alisema Loga .
“Nimeanza mchujo wa awali kwa kuwakata
hao lakini kazi hiyo inaweza kuendelea
kulingana na tutakachogundua mimi na
msaidizi wangu, hawa 26 tuliowachagua
tutaangalia watakavyokuwa wanajituma
katika mazoezi na hata mechi lakini kama
tutaona bado , tutapunguza wengine zaidi .”
Aidha , Loga ameonyesha kuchukizwa na
mgomo uliofanywa na beki wake Joseph
Owino ambaye amewaeleza viongozi wa
klabu hiyo kuwa hataweza kufika mapema
kama anavyotakiwa ambapo atatua nchini
Desemba 17 kama tiketi yake ya ndege
inavyomtaka huku Mzungu huyo akitamka
wazi kuwa , hatashindwa kumuondoa katika
kikosi hicho endapo hatafika mpaka Desemba
14.
“Nimeshtushwa na huyo beki kwa kusema
kwamba hataweza kufika mapema , lakini
najiuliza huko aliko anafanya nini wakati
nimesikia kuwa hata kwenye timu yake ya
taifa hayumo ? Sio sawa , nimesema mapema
kuwa atakayekosa nidhamu siyo mtu sahihi
kusalia Simba, labda mimi nisiwe kocha
hapa.
Hata hivyo , Loga ameshindwa kumuondoa
kipa kinda wa timu hiyo , Abuu Hashim ,
akisema atafanya hivyo haraka mara baada
ya Kamati ya Usajili ya Wekundu hao
kufanikisha kazi ya kumsaka msaidizi wa
Mghana, Yaw Berko mwenye uzoefu mkubwa.
Wachezaji ambao Loga amewapendekeza
kusalia Simba ni makipa Yaw Berko , Abuu
Hashim, mabeki wakiwa Issa Rashid , Omary
Salum, Haruna Shamte , Said Masoud
‘ Chollo’ , Joseph Owino , Hassan Hatib, Gilbert
Kaze, Miraji Adam.
Viungo ni Said Ndemla , Jonas Mkude, Henry
Joseph, William Lucian Abduhalim Humud,
Ramadhan Chombo , Amri Kiemba , Awadh
Juma , Uhuru Seleman , Haruna Chanongo ,
Ramadhan Singano ‘ Messi ’ wakati
washambuliaji ni Amissi Tambwe , Badru Ally,
Edward Christopher na Betram Mwombeki.

No comments:

Post a Comment

.