Sunday, December 8, 2013

Mchezaji Oljoro aula Sauz


Na Nicodemus Jonas
KIUNGO wa zamani wa maafande wa JKT
Oljoro, Yassin Juma Majota, amepata ulaji
katika Klabu ya Ajax Cape Town ya Afrika
Kusini ‘ Sauz ’ , baada ya kupewa nafasi ya
kufanya nayo mazoezi kwa kipindi cha miezi
miwili, kabla ya kusainishwa moja kwa moja .
Majota, 19 , aliyewahi kuitwa katika kikosi cha
timu ya taifa ya vijana , hadi anapata dili hilo,
alikuwa akiichezea Kinondoni FC baada ya
mkataba wake na Oljoro kumalizika msimu
uliopita .
Akizungumza na Championi Jumatatu,
Meneja wa Kinondoni FC, Saleh Alawi,
ambaye ndiye alimpeleka Sauz , alisema
mchezaji huyo kwa sasa ana wiki mbili tangu
aanze mazoezi na amekuwa akiendelea
vyema .
“Ana wiki mbili na anaendelea na mazoezi na
timu hiyo , sema tatizo bado hajapona vizuri
goti lake , hivyo anapewa mazoezi ambayo si
magumu zaidi , ikizingatiwa bado ni mdogo .
“Kuna matumaini akafuzu, maana baadhi yao
wanamjua uwezo wake, ndiyo maana
haikuwa kazi kuwashawishi . Tumuombee
apone kabisa goti na kusubiri

No comments:

Post a Comment

.