Watu watatu wanaosadikiwa kuwa majambazi
wameuawa kwa kupigwa na kuchomwa moto na
wananchi wenye hasira kali baada ya kudaiwa
kuvamia duka la bidhaa mbalimbali eneo la
Tabata Matumbi jijini Dar es Salaam kwa lengo la
kuiba.
Inadaiwa kwamba baada ya kumjeruhi muuza
duka na kushindwa kutumia bastola waliyokuwa
nayo majambazi hao wamejikuta wakikamatwa na
kuadhibiwa na wananchi hao.
ITV ikiwa katika eneo la tukio imeshuhudia
majambazi hao wakipigwa na kuchomwa moto
kabla ya polisi kufika na kuchukua miili ya
majambazi hao na kuipekela katika hospitali ya
taifa ya Muhimbili ikiwa imekwishaungua vibaya.
Friday, December 6, 2013
NEWZ ALERT,MAJAMBAZI YACHOMWA MOTO USIKU HUU ENEO LA TABATA MATUMBI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Daaah Mungu wangu
ReplyDelete