Saturday, December 7, 2013

NGAO : NAWASHANGAA


Nahodha wa kikosi cha Young Africans U20
- Issa Ngao .
Nahodha wa kikosi cha Young Africans U -20
ambaye pia msimu huu amepandishwa katika
kikosi cha kwanza Issa Rashid Ngao
amesema ameshangwaza na taarifa
zilizotolewa jana katika baadhi ya mitandao
kwamba yeye hana mkataba na Yanga na
kusema hizo ni taarifa za uongo .
Ngao ambaye katika mashindano ya Uhai
Cup yaliyomalizika mwishoni mwa wiki
aliibuka mchezaji bora wa mashindano hayo
amesema anashangazwa na taarifa hizo
ambazo hazina ukweli wowote na kwamba
yeye ni mchezaji wa Yanga kwa mkataba
ndio maana analipwa haki zake kila mwisho
wa mwezi .
Kiukweli hata mie nashangaa , sijui habari hizi
hata wamezitoa wapi , hawajaongea na mimi
kuweza kupata ukweli lakini cha ajabu hata
hawakuweza kuwauliza viongozi wangu.
" Mimi ni mchezaji wa U 20 Young Africans
kwa mkataba wa miaka miwili , nilisajiliwa
siku moja pamoja na wachezaji wenzangu
Rehani Kibingu , George Banda, Yusuph Abdul ,
Notikely Masasi na Mwinyi Bakari na wegine
wengi tu " alisema Ngao
Aidha Afisa Habari wa klabu ya Young
Africans Baraka Kizuguto amesema
ameshangwazwa na taarifa hizo ambazo
hazijafanyiwa upembuzi akinifu kabla ya
kutolewa kwa jamii, ukweli ni kwamba
wachezaji wote Yanga wana mikataba na
wanalipwa haki zao kila mwezi.
Hakuna mchezaji anayecheza bure Yanga
wala bila kuwa na mktaba na kama kuna
wanaojidanganya hivyo basi imekula kwao ,
vijana wote wa timu ya U 20 wanatambulika
na viongozi kwa ngazi zote kutokana na
kutambulika kwa ajira zao ndani ya Yanga.
Issa Rashid Ngao pamoja na kuwa ni
mchezaji wa timu zote za Yanga ya wakubwa
na vijana U 20, pia anaendelea na masomo
katika chuo kikuu cha Tumaini jijini Dar es
salaam akisomea Bachelor of Arts in
Education ( BAE ) akiwa mwaka wa pili sasa .

No comments:

Post a Comment

.