Saturday, December 7, 2013

MZEE MANDELA : NILIJIANDAA KUFA!


Ilikuwa Aprili 20, 2011 , Rais Mstaafu wa
Afrika Kusini , Nelson Rolihlahla Mandela
‘ Mzee Madiba ’ ( 95 ) aliyefariki dunia
Desemba 5, mwaka huu alirudia hotuba yake
ya mwaka 1964 aliyotoa akisema :
“Nilijiandaa kufa nikipigania demokrasia na
kupinga ubaguzi wa rangi . ”
Mzee Madiba aliirudia hotuba hiyo wakati
akiadhimisha miaka 47 tangu alipoitoa kabla
ya kufungwa jela miaka 27 na kuachiwa
mwaka 1990 .
Shujaa huyo wa Afrika na mtetezi wa watu
weusi duniani , alitoa maneno hayo katika
kituo chake cha kumbukumbu cha Nelson
Mandela ambacho nacho kilikuwa
kikiadhimisha miaka 47 tangu kuanzishwa
kwake.
Kiongozi huyo alisema alipanga ujumbe huo
uifikie dunia katika kipindi ambacho sasa
Mwafrika hatawaliwi kimabavu wala
kubaguliwa kwa rangi .
Alilenga katika kipindi chote, Mzee Madiba
tangu akiwa gerezani hadi alipotoka
hakuwahi kuirudia hotuba hiyo hadi Aprili 20,
2011 akiwa tayari ameanza kusumbuliwa na
maradhi ya mapafu .
Alisema: “Katika kipindi cha maisha yangu
nilijitolea mwenyewe kupigania Waafrika .
“Nimepigana kupinga utawala wa mabavu wa
watu weupe na nimepigana kupinga uonevu
wa mtu mweusi .
“Nimepigania demokrasia na upatikanaji wa
jamii huru ambayo kila mtu anapata haki na
usawa .
“Ndiyo maisha ambayo natumaini kuishi na
kufanikiwa lakini ikibidi nimejiandaa kufa. ”

No comments:

Post a Comment

.