Jana ndiyo ilikuwa siku ya mwisho kwa
wananchi wa Afrika Kusini na wageni kutoa
heshima zao za mwisho kwa Rais wa zamani wa
taifa hilo Nelson Mandela, baada ya kutengwa
siku tatu kwaajili ya zoezi la kuuaga mwili
wake uliowekwa katika ofisi za serikali jijini
Pretoria.
Watu waliojipanga mitaani wakati mwili
ukipelekwa Union Buildings kuagwa siku ya
mwisho
Ripoti zinasema umati mkubwa ulijitokeza
katika siku hizo tatu, na misululu ya watu
wapatao laki moja ilijipanga kwa umbali mrefu
wakisubiri kumuaga shujaa wao jana huku
wengine wakiambulia kuuona tu katika gari.
Polisi wakijaribu kuwazuia watu wasiendelee
kuingia
Kutokana na umati mkubwa uliojitokeza, polisi
walijaribu kuzuia watu wasiendelee kuingia kwa
kufunga mageti, lakini hata hivyo watu hao
walilisukuma na kutaka kuingia kwa nguvu ili
na wao wakatoe heshima zao za mwisho.
Katika vurugu hizo baadhi ya waombolezaji
walianguka na kukanyagana, baadhi yao
walipata majeraha madogo.
Huko kijijini Qunu ambako mwili wa Mandela
unatarajiwa kupelekwa leo tayari kwa mazishi
yatakayofayika kesho Jumapili, maandalizi
yako katika hatua za mwisho.
Qunu, maandalizi ya mwisho yakifanywa tayari
kupokea mwili kwa mazishi kesho
Siku ya Jumatatu (December 16) baada ya
mazishi, Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma
anatarajiwa kuzindua sanamu ya Nelson
Mandela, ambayo imeonekana ikimaliziwa
kuwekwa katika ofisi za Serikali ‘Union
Buiildings’ jijini Pretoria jana.
Sanamu ya Mandela ikimaliziwa
Friday, December 13, 2013
PICHA; WATU 100,000 WAJITOKEZA KUUWAGA MWILI WA MANDELA, WENGINE WAUMIA WAKIGOMBANIA KUMUAGA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
mm ndo Mandela nikaefata
ReplyDelete