Stori: Brighton Masalu
SINEMA ya madai mazito dhidi ya mastaa wa
filamu Bongo, Blandina Chagula ‘Johari’, Ruth
Suka ‘Mainda’ na Chuchu Hans ambaye ni mke
wa mtangazaji Frank Mtao kuchanganywa
kimapenzi na Vincent Kigosi ‘Ray’ sasa
inaendelea na mhusika mkuu Ray amefunguka
na kueleza yake ya moyoni huku akisisitiza:
“Chuchu ndiye mke wangu, tarajieni makubwa
soon (hivi karibuni).”
Akizungumza na Risasi Mchanganyiko, wikiendi
iliyopita katika Viwanja vya TCC Chang’ombe
jijini Dar es Salaam ambapo kulikuwa na mechi
kati ya wasanii wa Bongo Fleva na Bongo Muvi,
Ray aliwashangaa waandishi kwa kumshambulia
kutoka kimapenzi na Chuchu.
Mwandishi wetu alianza kwa kumwuliza: “Ray
magazeti yanaandika kuhusu wewe kutoka na
Chuchu Hans ambaye ni mke wa mtu. Mainda
amezungumza mengi. Kukaa kwako kimya bila
kufafanua chochote siyo kitu kizuri. Tafadhali,
hebu zungumza japo kidogo kuhusu madai ya
Mainda.”
RAY: Sikia nikuambie, huyo Mainda utoto
unamsumbua. Haniumizi kichwa kabisa. Kuhusu
Chuchu... si mmeshaandika? Endeleeni kuandika
lakini soon mtashuhudia kitu kikubwa sana.
RISASI: Ni kitu gani hicho?
RAY: Niacheni na Chuchu wangu.... kifupi ndiye
mke wangu na itawashangaza wengi. Halafu
mimi nawashangaa sana. Yaani mimi kutoka na
Chuchu mnakuzaaaa... mbona alivyokuwa na
ma-boyfriend zake wengine hamkuandika? Kwa
sababu ni Ray basi mkaona ni habari. Mimi
ninavyojua Chuchu siyo mke wa mtu.
Kwanza mimi sijamchukua kutoka mikononi mwa
mumewe kama mnavyosema. Chuchu tayari
alikuwa na maisha yake mapya. Nilimchukua
kutoka kwa Libert (hajafafanua zaidi ni nani).
Mbona alivyokuwa na huyo Libert hamkuandika?
Kifupi niacheni na maisha yangu.
RISASI: Vipi kuhusu Johari?
RAY: (Huku akikimbia kuingia uwanjani) Tena
huyo mama yako (akimuonesha mwandishi
Johari) anakuja.
Mwandishi wetu aliachana na Ray aliyekuwa
akiingia uwanjani na kumfuata Johari lakini
hakuwa tayari kusema chochote achilia mbali
hata kumsikiliza mwandishi wetu!
TUJIKUMBUSHE
Hivi karibuni gazeti hili liliandika habari yenye
kichwa MAINDA: NIMETOA MIMBA YA RAY.
Ndani yake Mainda alifunguka mengi ikiwemo
kuchanganywa kimapenzi na Ray, yeye na
wenzake Johari na Chuchu Hans.
GPL
Wednesday, December 4, 2013
RAY "JOHARI NA MAINDA TUPA KULE CHUCHU HANS NDIO MKE WANGU"
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment