Thursday, December 5, 2013

SINEMA YA BABY MADAHA NA DIAMOND BADO INAENDELEA,DIAMOND NAE AFUNGUKA NA KUMPONDA BABY MADAHA


ACHANA na mabifu yaliyotangulia, hili ni jipya
kabisaa! Msanii wa sinema na Bongo Fleva, Baby
Joseph Madaha ameingia kwenye bifu zito na
Nasibu Abdul Jumaa ‘Diamond Platnumz’ na
kudai staa huyo wa Wimbo wa Number One ni
mzinzi ‘fuska’, Amani lina mkanda mzima.
Bila kumung’unya maneno, mapema wiki hii,
Baby Madaha alimvaa Diamond ambaye ni Rais
wa Wasafi Classic Baby (WCB) akimtuhumu
kuwa na tabia za kifuska.
Baby Madaha alidai hata muziki anaoufanya
Diamond kamwe hauwezi kulingana na mafanikio
makubwa ya jina lake zaidi ya kubebwa na
skendo tu.
CHOKOCHOKO ZILIVYOANZA
Kupitia mitandao ya kijamii, ilivuja posti ambayo
ilidaiwa kutoka kwa Baby Madaha ikimpaka
Diamond kuwa siyo mwanamuziki kama ilivyo
kwa wasanii wengine wenye uwezo mkubwa,
akitolea mfano Elias Barnaba wa THT.
Sehemu ya posti hiyo ilionesha kuwa, Diamond
si msanii wa muziki bali ni mzinzi f’lani hivi
anayefanya biashara ya muziki kupitia mapenzi.
“Siku wanawake maarufu nchini Tanzania
watakapojitambua na kuacha kulewa penzi la
Diamond, huo ndiyo utakuwa mwisho wa maisha
yake kimuziki kwa sababu hatakuwa na jipya na
hivyo soko lake litaporomoka,” ilisomeka posti
hiyo.
UKWELI NI UPI?
Baada ya ishu hiyo kugeuka habari ya mjini na
kuibuka kwa makundi mawili yanayokinzana,
Amani lilimtafuta Baby Madaha ili kujua ukweli
wa posti hiyo ndipo akatiririka aya za
kuthibitisha kuwa picha haziivi, hamkubali
Diamond na kudai hata kimuziki hamkubali kwani
anaamini wapo wanamuziki wanaofanya vema
katika gemu kuliko yeye.
“…tuseme ukweli, Diamond ni mfanyabiashara
siyo mwanamuziki. Kuhusu hiyo posti iwe ni
mimi nimeandika au si mimi lakini kimsingi hayo
maneno yanamstahili kabisa. Mzinzi tu.
“Diamond anabebwa na media (vyombo vya
habari). Kuna wanamuziki wengi wazuri sembuse
yeye? Ana nini haswa?” alihoji Baby.
AMANI LAMGEUKIA DIAMOND
Baada ya kusikia maelezo ya Baby kwa kifupi,
Amani lilimuweka ‘pending’ kwa muda na
kumwendea hewani Diamond ili liweze kujua
upande wake analizungumziaje bifu hilo ambalo
lilikuwa likienea mitandaoni kama moto wa kifuu.
Tofauti na matarajio ya mapaparazi wetu
kwamba huenda angejibu mashambulizi makali
kwa Madaha, Diamond au ‘Sukari ya Warembo’
aling’aka huku akimponda mwanadada huyo na
kumshangaa:
DIAMOND SASA
“Daaah! Huko ni kunishusha…mimi na huyo
(Baby) wapi kwa wapi kamwe huwezi
kunilinganisha na mtu ambaye yupo chini yangu
sana, nikijibizana naye nitajishusha tu. Ingekuwa
ni mtu mkubwa mwenye levo yangu hapo
ningesema natakiwa kusema neno.
“Hana lolote huyo anatafuta ‘kiki’ tu kupitia
mimi, nipo na dili zangu za maana nipoteze
muda kwake? Atafute wa levo yake na wala si
mimi.”
UZINZI VIPI?
Alipoulizwa kuhusu suala la uzinzi ambalo Baby
Madaha aliumaanisha katika posti yake,
Diamond aliendelea kukazia kuwa hana muda wa
kupoteza kwa mtu kama Baby Madaha ambaye
kimsingi ni kama ardhi na mbingu.
“Huyo anatafuta kiki tu, aachane na mimi…
mbona hatufanani kabisa mimi na yeye wapi
kwa wapi?” alikazia Diamond a.k.a Weka Mbali
na Watoto Wazuri wa Kike.
BABY AREJEA HEWANI
Wakati mapaparazi wetu wakimalizana na
Diamond, kilongalonga kimoja cha paparazi wetu
kilikuwa kikionesha kinaita, ilivyokatika ya
Diamond, Baby akapanda hewani kwa mara
nyingine.
Safari hii alimchana laivu: “Nimeisoma upya
posti yenyewe, kilichopo humu ni ukweli mtupu.
Hakuna hata tone la uongo, wewe
utamlinganisha Diamond na mtu kama Barnaba?
Huyu ni mfanyabiashara tu, hajui kuimba kwa
kutumia vyombo kama mimi.
“Diamond hawezi kupiga chombo hata kimoja
cha muziki atajiitaje mwanamuziki? Anastahili
kabisa ujumbe huu.”
UFUSKA
Mapaparazi wetu walilazimika kumtwanga swali
Baby Madaha kuhusiana na ufuska ambao
ulikuwa umetajwa katika maelezo ya awali,
kama endapo Diamond ni mzinzi au yeye ndiyo
mzinzi.
Katika maelezo yake, Baby Madaha
aliwashangaza mapaparazi wetu kwa kutaja
namna gani anaweza kumuita Diamond mzinzi.
Sikia:
Amani: “Umesema Diamond si mwanamuziki, je,
suala la uzinzi ni nani analo kati yako na yeye?”
Baby: “Mimi si mzinzi. Diamond ndiyo mzinzi
tena sana tu.”
Amani: “Uzinzi wake upo wapi?”
Baby: “Kitendo cha kubadilisha wanawake,
kufumaniwa na Wema Sepetu akiwa na Jokate
Mwegelo ndiyo uzinzi wenyewe huo.”
Amani: “Kwani wewe hujawahi kuwa na
wanaume tofauti? Hujawahi kufumaniwa?”
Baby: “Mimi sijawahi, yeye amewahi na
hakuwahi kukanusha hivyo inadhihirisha kuwa ni
kweli. Kwangu mimi kila aliyetajwa kutoka na
mimi kama haikuwa kweli, nilikanusha mara
moja yeye mbona hakanushi?”
Amani: “Kwani Diamond alifumaniwa na nani?”
Baby: “Acha hizo, kwani hukumbuki kipindi cha
Wema? Mara alinaswa na Aunt mara na… yule
ndiyo mzinzi sasa.”
KWANI WALITONGOZANA?
Kuhusu suala la kutongozwa, Baby alisema
Diamond hajawahi. Cha kushangaza zaidi,
alisema hata kama ikitokea siku staa huyo
akamtongoza kamwe hawezi kumkubalia kwani
hawaendani hata kidogo.
Alisema yeye ni mtu wa kutembea na vigogo na
si vitoto kama Diamond.
“Hana hela, kamwe siwezi kumkubalia. Ni mtu
ambaye ana vihela mbuzi sasa mtu kama yeye
mimi wa nini? Ndiyo maana aliwahi kukimbiwa
na mwanamke kwa kuwa hana hela.
“Tena yule mwanamke akaenda kwa kigogo
mwenye hela, mimi na yeye ni mbalimbali
kabisa. Hata muziki ninaofanya hauwezi, mimi
ninaimba RnB yeye anafanya Pop, tuko tofauti
kabisa,” alisema Baby pasipo kumtaja
mwanamke aliyemkimbia Diamond.
TUJIKUMBUSHE PANDE ZOTE
Diamond aliwahi kuripotiwa kutoka kimapenzi na
‘totoz’ kibao wakiwemo yule wa mwanzo
aliyemzingua aitwaye Sarah, Rehema Fabian,
Jacqueline Wolper, Upendo Mushi ‘Pendo wa
Maisha Plus’, Wema Sepetu, Natasha (Video
Queen wa Wimbo wa Moyo Wangu), Najma
(aliwahi kuwa mpenzi wa Mr. Blue), Jokate
Mwegelo, yule demu wa Kenya na aliyekuwa
mwigizaji aliyefulia ambaye ni mke wa mtu.
Kwa upande wake Baby Madaha anayekimbiza
na ngoma yake ya Summer Holiday

No comments:

Post a Comment

.