Siku kadhaa tu baada ya B hits kusema haitotoa
msamaha kwa wasanii wake ambao ni Vanessa
Mdee, Gosby na Mabeste kutokana kufanya mambo
nje ya mkataba pamoja na utovu wa nidhamu,
kampuni hii iliyohusika kutoka hits kadhaa za
bongofleva imetoa tamko kuhusu nyimbo za Gosby
na Vanessa ambazo zimeachwa kwenye studio hiyo
waliyokua wakifanya kazi.
Amani ambae ni msemaji wa B Hits anasema ‘hizo
nyimbo ziko hapa, Gosby ndio ana nyimbo nyingi
kuliko Vanessa na hatuko tayari kuwapa.. pia kuna
swali kubwa ambalo watu wengi wanauliza kwa
nini B Hits haikai na Wasanii na kila mara
inakorofisha… sababu kubwa ya Wasanii wengi
kuondoka B Hits ni hii mikataba tuliyoitengeneza’
Studio ya B hits mpaka sasa imeshatengeneza hit
single kama ‘Closer’ ya Vanessa Mdee, ‘habari ndio
hiyo’ ya FA & Ay pia ‘nangoja ageuke’ na single
nyingine kadhaa.
Wednesday, December 4, 2013
SOMA WALICHOKISEMA B HITS KUHUSU KUWAPA AU KUTOWAPA NYIMBO ZAO KINA VANESSA NA GOSBY. SOMA HAPA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment