Thursday, December 12, 2013

TINO AFUNGUKA "FILAMU ZA BONGO HAZIUZI BILA KUTUMIA WASICHANA WAREMBO

.
Bila wasichana warembo kwenye filamu ya
kibongo, hakuna atakayeinunua na huenda
waandaaji wakaishia kuiangalia tu nyumbani na
familia zao.
Kwa mujibu wa Tino, wasichana warembo ni
‘chambo’ kinachowavuta wanunuzi wa filamu za
Tanzania. Ujuzi wa uigizaji na kipaji, si sababu
kwao.
Akiongea na gazeti la Mwanaspoti, Tino alisema
warembo hao pamoja na kuzifanya filamu
zivutie pia huwa na juhudi katika kazi hiyo
tofauti na wanaume na wanaipenda kazi yao.
“Kwa kweli bila kuweka wasichana warembo
katika filamu yako hutauza kwa sababu wengi
wana juhudi za kufanya mambo mapya kila
kukicha, lakini pia wanakuongezea mvuto kwa
kuwa warembo ni kama maua,”alisema Tino.
Pengine ndio maana waigizaji wa kike
wanaotamba ni walewale akina Wema Sepetu,
Lulu, Irene Uwoya, Jacky Wolper, Batulli na
wengine waliojaaliwa sura za kuvutia

2 comments:

.