MICHUANO ya timu za bandari nchini leo
inatarajiwa kufunguliwa rasmi katika viwanja
vya TCC Sigara, huku jana baadhi ya timu
zikianza kwa ushindi michezo hiyo .
Katika michezo ya utangulizi iliyofanyika
jana, katika upande wa kikapu Makao Makuu
imeanza vyema baada ya kuwachapa wenzao
wa Tanga kwa vikapu 55 kwa 46 , katika soka
Mwanza walichomoza kwa ushindi wa mabao
2-1 dhidi ya Mtwara .
Katika mchezo huo mabao ya Mwanza
yakifungwa na Ernest Kijika dakika ya saba
na Revocatus Makonda akifunga la ushindi
dakika ya 27 wakati lile la Mtwara likifungwa
na Semu Timilay dakika ya 63 .
Katika mchezo mwingine wa pete , Tanga
ilianza vyema katika upande huo baada ya
kuwachapa Mtwara kwa magoli 36- 13,
ambapo leo michuano hiyo itafunguliwa
rasmi katika viwanja hivyo vya Sigara baada
ya jana kushindikana kutokana kuingiliana
kwa ratiba ya mgeni rasmi .
Tuesday, December 10, 2013
Ufunguzi michezo ya Bandari leo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment