KOCHA Mkuu wa Simba, Zdravok Logarusic ,
amesema washambuliaji wa timu hiyo ,
akiwemo Betram Mwombeki, hawajamridhisha
na kuagiza uongozi kumtafutia watu makini
zaidi .
Akizungumza na Championi Jumatano ,
Logarusic maarufu kwa jina la Loga,
amesema Mwombeki ni mshambuliaji mzuri
wa wastani , ambapo kikubwa ambacho
ameshindwa kukikubali ni jazba zake
uwanjani na kutaka uongozi wa Wekundu hao
kusaka mtu makini zaidi atakayesaidiana na
Amissi Tambwe .
Loga ambaye ni beki wa zamani wa kushoto
wa Croatia , amesema tayari kazi hiyo
ameshawakabidhi viongozi wa Simba,
ambapo amesisitiza kama aina hiyo ya
mshambuliaji anayemtaka akipatikana ,
Wekundu hao watakuwa na safu kali ya
ushambuliaji.
“Nimefanya kazi ya kuwaangalia kwa makini
washambuliaji waliofika mpaka sasa , kidogo
huyu Betram ( Mwombeki) anaonekana kuna
kitu anacho, lakini tatizo moja alilonalo ni
jazba akiwa uwanjani, sijajua ni mazoezini tu
au hata kwenye mechi , ” alisema Loga .
“Nimewaambia viongozi kwamba kama
wataweza waniongezee mshambuliaji mmoja
mzuri zaidi ya huyu, ambaye atashirikiana na
Amissi ( Tambwe ) , ambaye nimepata sifa zake
kwamba ni mtu makini kwenye kutekeleza
majukumu yake ya ufungaji , nataka ubingwa
hapa, ” alisema Loga .
Tuesday, December 10, 2013
Logarusic aagiza straika mpya Simba
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment