Jumatano ya wiki hii muigizaji mrembo wa
Bongo Movie Wastara Juma, alikuwa mgeni
katika kipengele cha ‘Kikaangoni Live’ ya EATV,
ambayo mtu maarufu huchat live na mashabiki
wake kupitia ukurasa wa EATV.
Urembo wa muigizaji huyo huenda ndio chanzo
cha mishale mingi ya maswali kutoka kwa
mashabiki wa Wastara, waliokuwa na kiu ya
kutaka kufahamu baada ya kumpoteza mume
wake Sajuki, hivi sasa ni mwanaume gani
mwenye bahati ambaye yuko katika kisiwa chake
cha ‘makopa’, yaani mpenzi wake wa sasa.
“Inshort mimi nina watoto watatu ambao
wananiangalia wao zaidi kuliko kitu chochote”
huo ndio ulikuwa mwanzo wa jibu la maswali
hayo kutoka kwa Wastara.
“Kikubwa nachokifanya sasa hivi ni kuangalia
watoto wangu na kuwawekea misingi mizuri
kama kuna kitu ambacho nilimiss wakati niko
kwenye matatizo na mpaka mume wangu
kufariki , basi naangalia jinsi ya kukirudisha
katika hali yake ya kawaida, lakini swala la
mahusiano silipi kipaumbele”. Alisema Wastara
alipozungumza na E-News ya EATV baada ya
‘Kingaangoni Live’.
Akizungumzia career yake ya uigizaji Wastara
amedai kuwa mashabiki wake watarajie movie
zake nyingi zitakazotoka mwakani , sababu kwa
mwaka huu tunaoumaliza amefanikiwa kufanya
filamu saba ndani ya miezi sita, kitu ambacho
hakuwahi kufanya toka ameanza uigizaji.
“Mimi sijawahi kufanya movie hata mwaka
mmoja toka nimeanza kufanya sanaa kama
mwaka huu, nimefanya movie saba…ni movie
nyingi sana kwangu, kwasababu sijawahi”.
Alimaliza Wastara.
Kwa sasa movie mpya ya Wastara iliyoko sokoni
inaitwa ‘Shaymaa’.
Friday, December 13, 2013
WASTARA AFUNGUKA LIVE KUHUSU MAHUSIANO YAKE YA KIMAPENZI PAMOJA NA KAZI ZAKE..!!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
WASTARA WA MIYE
ReplyDeleteWASTARA WA MIYE
ReplyDeletehehehe othman bana nlijua tu
ReplyDeletemungu amsaidie kufikia malengo yake
ReplyDeletena amuondolee mikosi.
Ameen
Kama namuona anajibu analia wastara
ReplyDeletemungu akuongoze ktk kaz zako na kushinda mabaya haswa pepo la ngono kwa wsanii maana washaona ni dili kwenye vyombo vya habar
ReplyDelete