Stori: Imelda Mtema na Richard Bukos
KICHEKO! Ile kesi ya kumpiga na kumtukana
matusi ya nguoni Meneja wa Hoteli ya
Mediteranian iliyopo Kawe Beach, Dar ,
Godlucky Kayombo iliyokuwa ikimkabili Wema
Isaac Sepetu imetolewa hukumu yake kama
ilivyokuwa ile ya shosti ’ ake , Kajala Masanja .
Wema Sepetu akitinga Mahakama ya
Mwanzo ya Kawe , Dar .
Habari kutoka kwa chanzo makini cha gazeti
hili kilieleza kuwa Wema alihukumiwa kifungo
cha miezi mitatu au faini ya shilingi laki moja
kwa maana ya elfu hamsini kwa kila kosa
baada ya kukutwa na hatia ya kutenda
makosa hayo mawili ya kupiga na kutukana .
WEMA AOMBA IHARAKISHWE
Habari za ndani kutoka kwa mtu wa karibu
wa Wema au Madam zilieleza kuwa hukumu
ya kesi hiyo ilikuwa iahirishwe lakini staa
huyo akaomba itolewe kwa kuwa alitaka
kusafiri.
Ilisemekana kuwa mbali na kuwa na safari
pia aliomba itolewe kwa sababu yupo ‘ bize ’
na maandalizi ya arobaini ya baba yake,
Isaac Sepetu aliyeaga dunia hivi karibuni .
Hukumu hiyo ilitolewa katika Mahakama ya
Mwanzo ya Kawe, Dar ambako ndiko kesi
hiyo ilipokuwa ikirindima tangu mwezi Agosti,
mwaka huu .
Wema Sepetu na rafiki zake wakijadiliana
jambo eneo la Mahakama ya Mwanzo ya
Kawe , Dar .
ASUBIRIWA KUPELEKWA GEREZANI ,
ACHOMOA ‘ MADOLARI’
Ilielezwa kuwa katika hukumu hiyo
iliyosomwa kwa takriban saa mbili , Wema
alikuwa akisubiriwa nje tayari kupelekwa
gerezani lakini kama kawaida yake fedha
iliongea ambapo alizamisha mkono laini
kwenye ule mkoba wake na kuchomoa
‘ madolari’ .
Chanzo kilidai kuwa zilihitajika fedha za
Kibongo hivyo Wema alichambua mkoba
wake na kutoa ‘ wekundu ’ kumi huku
akirejesha zile dola za Kimarekani.
“Wema alifanya kama alivyomfanyia Kajala
siku ile pale Kisutu. Kwa Wema ishu ya fedha
siyo tatizo sana . Kuliko kumpotezea muda ,
Wema yupo tayari kutoa kiasi chochote cha
fedha.
“Kwa Wema muda ni kitu cha muhimu zaidi
kuliko hata hiyo fedha ndiyo maana alitoa tu
hiyo faini mara moja , ” kilisema chanzo hicho.
Baada ya kupokea maelezo hayo, gazeti hili
lilimsaka Wema ili kupata mzani wa habari
hiyo lakini simu yake iliita bila kupokelewa.
Wema na shosti wake Kajala wakitoka
mahakamani hapo .
Hata hivyo , alipotafutwa meneja wake , Martin
Kadinda na kuulizwa juu ya suala hilo
alifunguka:
“Ile kesi iliisha tangu Ijumaa iliyopita, watu
hawakujua tu . Wema alihukumiwa kifungo
cha miezi mitatu au faini ya shilingi laki
moja.
“Alichokifanya Wema alilipa faini hiyo na
sasa yupo freshi na mishe zinaendelea .
Unajua haruhusiwi kufanya mahojiano hadi
amalize arobaini ya baba yake. ”
Chanzo kilisema kuwa kabla ya hukumu hiyo ,
Wema alikuwa katika hali kama ile iliyomkuta
Kajala wakati wa hukumu yake miezi kadhaa
iliyopita kwani alikuwa akilia , kujuta na
kumuomba Mola amuepushe na balaa hilo
lililosababishwa na kuwa ‘ tilalila’ .
Hata hivyo , hukumu hiyo iliwashangaza watu
kwani iliendeshwa kwa muda mrefu na kwa
mbwembwe nyingi lakini hokumu yake ikawa
ya kawaida tofauti na matarajio ya wengi .
Wema Sepetu na kampani yake wakiondoka
eneo la m ahakama.
KAJALA NAYE KICHEKO TENA
Wakati Wema akikenua , wiki hii Kajala naye
ilikuwa chereko chereko baada ya
Mahakama ya Rufaa Kanda ya Dar kuridhika
na hukumu yake iliyotolewa na Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kisutu mapema mwaka huu
kufuatia rufaa iliyokatwa na mume wa staa
huyo Faraji Chambo .
Katika kesi ya awali , Kajala alihukumiwa
kifungo cha miaka mitano au faini ya Sh .
milioni 13 baada ya kupatikana na hatia ya
kushirikiana na mumewe kwenye msala wa
kutakatisha fedha haramu wakati mwanaume
huyo akifanya kazi Benki ya NBC , Dar .
Hata hivyo , Wema alimlipia faini hiyo kama
alivyofanya kwenye kesi yake.
Katika hukumu ya rufaa hiyo , majaji
walijiridhisha kwamba kesi hiyo iliendeshwa
ipasavyo na Kajala alitimiza taratibu za kuwa
huru kwa kulipa faini lakini mumewe
aliyehukumiwa miaka saba alishindwa kulipa
faini ya Sh . milioni 213.
MAOMBI YAO YASIKIKA
Wema na Kajala wamekuwa kwenye maombi
ya kufunga wakisali na kufanya dua ili
kuwaepusha na kifungo hivyo kwa sasa wote
ni vicheko.
Thursday, December 5, 2013
WEMA YAMKUTA YA KAJALA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Shuhuri mbona
ReplyDelete