Sunday, December 8, 2013

WOLPER MAJANGA !


Jacqueline Wolper Massawe.
Stori: Gladness Mallya
SEXY lady katika tasnia ya filamu za
Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe
amepata majanga baada ya gari lake
kugonga gari lingine na vitu kibao kwenye
siku ya ‘ bethidei’ yake .
Pichani ( chini kushoto) ni gari aina ya
Toyota Prado lililogonga gari lingine kulia
pamoja na matenki ya maji na mabomba .
Tukio hilo lilijiri Ijumaa iliyopita nyumbani
kwake Mwananyamala , Dar akiwa anasogeza
lile gari lake jipya aina ya Toyota Prado ili
lioshwe ambapo aliponea chupuchupu kuuvaa
ukuta .
Habari zilieleza kuwa Wolper , badala ya
kukanyaga breki alijikuta akikanyaga mafuta
na kusababisha abomoe matenki ya maji na
kupasua mabomba yote pia kugonga gari
lingine lakini hakuumia ila presha ilishuka
kidogo.
“Kuzaliwa ni siku moja na kufa ni siku moja
ndiyo maana kila siku nasisitiza upendo na
tuache chuki zisizokuwa na sababu.
“Leo ( Ijumaa ) nilikuwa nauvaa ukuta ikiwa
ndiyo kwanza naanza maandalizi ya
kusherehekea bethidei yangu , nimebomoa
matenki na nimepasua mabomba lakini yote
namshukuru Mungu kwa kuwa sijaumia,
asante Mungu wa wote kimbilio la wote na
wewe ndiyo kimbilio langu , niombeeni
jamani, ” aliandika Wolper katika akaunti yake
ya Instagram .

1 comment:

  1. Huyu nae siku hizi anajipeleeeka kupata umaarufu kwa magazetii story kaiuzaa

    ReplyDelete

.