Stori: Joseph Ngilisho , Arusha
OOH my God! Kikongwe mwenye umri wa
miaka 105 , Nembris Mollel , mkazi wa Moivo-
Sanawari mkoani hapa anadaiwa kuuawa
kinyama kwa kukatwa mapanga kichwani na
mtu anayedaiwa kuwa fundi ujenzi mwenye
umri kati ya miaka 35 na 40 kisa kikielezwa
ni mapenzi.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo,
baada ya kutenda unyama huo, wananchi
wenye hasira walimvamia mtuhumiwa na
kumpa kichapo ‘ hevi ’ hadi alipookolewa na
askari, akapelekwa Hospitali ya Mkoa wa
Arusha, Mount Meru alikolazwa.
Taarifa zilizothibitishwa na jeshi la polisi
mkoani hapa zilieleza kwamba kikongwe huyo
aliuawa majira ya saa 4: 30 asubuhi akiwa
anaota jua nyumbani kwake.
Majirani wa bibi huyo walidai kuwa fundi
ujenzi huyo amekuwa akimtaka kimapenzi
kikongwe huyo kwa muda mrefu ambapo
alitoa taarifa kwa mjukuu wake aitwaye
Jonas Sanin ’ go.
Kwa mujibu wa shuhuda aliyejitambulisha
kwa jina la Emanuel Kiria, alimuona
mtuhumiwa akiwa na panga bila kujua
anaelekea wapi lakini muda mfupi baadaye
alimshuhudia akimkata kikongwe huyo
kichwani zaidi ya mara tatu na kujaribu
kutoroka.
Kutokana na tukio hilo, wananchi
wameliomba jeshi la polisi mkoani hapa na
vyombo vya dola kwa jumla kushughulikia
chanzo cha tukio hilo kwani taarifa nyingine
zilidai kuwa mtuhumiwa alikuwa na matatizo
ya akili huku wengine wakidai alikuwa na
mpango wa kumbaka kikongwe huyo.
Kamanda wa polisi mkoani hapa , Liberatus
Sabas alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na
kueleza kuwa polisi wanafanya uchunguzi ili
kubaini chanzo chake .
Mwili wa marehemu ulihifadhiwa katika
chumba cha maiti kwenye Hospitali ya Mount
Meru ukisubiri mazishi huku mtuhumiwa
akipatiwa matibabu hospitalini hapo akiwa na
pingu akisubiri kufikishwa kwa pilato .
Sunday, December 8, 2013
KIKOGWE MIAKA 105 AUAWA KISA MAPENZI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Mtu kama akutakii kumuua ndo anakubar
ReplyDelete