Marehemu Nelson Mandela enzi za uhai
wake .
Mwandishi Wetu na Mitandao
WOSIA aliowahi kuuandika hayati Nelson
Rolihlahla Mandela ‘ Mzee Madiba ’ au
‘ Tata ’ ( 95 ) enzi za uhai wake akielezea
anavyotaka azikwe , ndiyo tishio kubwa lenye
utata kuelekea siku ya mazishi yake,
Jumapili ijayo , Ijumaa Wikienda limebaini.
Mtandao mmoja nchini humo
umeukumbushia wosia huo huku familia
ikianza kuonesha misimamo tofautitofauti,
hali inayoashiria kuibuka kwa makundi mawili
yanayokinzana .
Gari lililobeba mwili wa Nelson Mandela .
FAMILIA INAVYOTAKA
Habari za ndani zilisema kuwa familia
inataka mazishi ya kiongozi huyo maarufu
duniani yawe makubwa na ya kisasa kwa vile
viongozi wa nchi mbalimbali duniani
watahudhuria .
“Mandela ni kingozi mkubwa sana duniani,
mazishi yake lazima yawe makubwa pia ya
kisasa. Hawezi kuzikwa kama mwananchi wa
kawaida , ” ilisomeka sehemu ya taarifa hiyo .
Mmoja wa waombolezaji akigusa picha na
Mandela .
Taarifa hiyo iliongeza kuwa wakati familia
hasa wajukuu na watoto wake wakishikilia
msimamo huo , wapo wanandugu wanaotaka
azikwe kama alivyoandika katika wosia wake
huo.
SERIKALI YAPANGA MAMBO BILA KUFUATA
WOSIA
Habari zaidi zilisema kuwa Serikali ya Afrika
Kusini inajitahidi kuupangua wosia huo kwa
kuendelea na maandalizi ya mazishi kama
haukuwahi kuwepo licha ya kwamba jamii ya
watu nchini humo inaheshimu wosia wa
marehemu.
WOSIA UNAVYOSEMA
Mzee Madiba alishauandika wosia huo
kwenye karatasi moja tu ambapo aliagiza
anavyotaka azikwe . Alisema kuwa akifa
azikwe katika milima iliyojitenga nyumbani
kwa mababu zake katika Kijiji cha Qunu ,
Eastern Cape huko ‘ Sauzi ’ .
Waombolezaji wakiweka maua katika
sanamu la Mandela .
ALITAKA MAZISHI YA KAWAIDA SANA
Inadaiwa wosia huo aliuandika Januari , 1996
wakati bado akiwa rais ambao ulijaa
maelekezo yote juu ya mazishi yake . Aliagiza
kufanyiwa mazishi ya kawaida sana yenye
hadhi ya raia wa kawaida nchini humo hivyo
kuyafanya kuwa makubwa na ya kifahari ni
kukiuka wosia wa mzee .
KABURI ALILOLITAKA MANDELA
Katika wosia wake huo uliotolewa na rafiki
yake wa karibu , Mzee Madiba aliandika kuwa
akifa azikwe katika eneo la familia lenye
makaburi ya ukoo wa Mandela kijijini hapo .
Pia aliagiza kuwa kaburi lake liwekewe jiwe la
kawaida kama alama ya mahali lilipo ili lisije
kupotea kwa mvua au mabadiliko ya tabia
nchi .
Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma .
KABURI LISISAKAFIWE
Katika tafsiri ya maneno hayo, Mzee Madiba
alitaka kaburi lake liwe la kawaida sana,
akimaanisha lisijengewe kama ilivyokuwa
kwa makaburi ya viongozi wengine wa mfano
wake barani Afrika kama , Mwalimu Julius
Nyerere wa Tanzania na Kamuzu Banda
( aliyekuwa Rais wa Malawi) .
WOSIA WAKE ULIKUWA WA UPANDE
MMOJA WA KARATASI
Magazeti ya nchini humo , South African Mail
na Guardian miezi ya karibuni yaliripoti
kumnukuu rafiki huyo wa siku nyingi wa
familia ya Mandela akisema : “Madiba
hakuwahi kukifanya kifo kuwa jambo kubwa
la kufikiriwa , pia hakuwahi kutaka chochote
cha fahari wakati wa kumzika .”
Cha ajabu , wosia huo wa Mandela ulitosha
kwenye upande mmoja wa karatasi ya
kawaida ya kuandikia licha ya kwamba
mauzo ya kitabu chake cha L
Sunday, December 8, 2013
WOSIA WA MANDELA WAZUA UTATA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment