Thursday, January 2, 2014

BABY MADAHA AMSHIKA UCHAWI DIAMOND


Na Mayasa Mariwata
STAA wa muziki wa Bongo Fleva, Baby Joseph
Madaha ‘ amemshika uchawi ’ msanii
mwenzake , Nasibu Abdul ‘Diamond’ kufuatia
madai kuwa , kuna msanii maarufu Bongo
alikwenda kwa mganga wa kienyeji Tanga
akitaka kumfanyizia ‘ madongoloji ’ mrembo
huyo ili mambo yake yaende ndivyo sivyo.
Nasibu Abdul ‘ Diamond’.
ILIKUWAJE KWANI ?
Desemba 22 , mwaka jana , mtu mmoja
aliyedai ni sangoma aishiye Tanga mjini
alituma ujumbe mfupi wa maneno ( SMS)
kupitia simu ya chumba cha habari Global
akiomba namba ya Baby Madaha.
Mtu huyo alisema anaomba namba hiyo kwa
sababu kuna mtu alikwenda kwake (Tanga)
akitaka amfanyizie Baby Madaha mambo
yaende kombo .
Baby Madaha.
NAMBA YA BABY MADAHA YARUSHWA
Baada ya meseji hiyo kusomwa, mtu huyo
alirushiwa namba ya Baby Madaha kisha
ujumbe wake ukafowadiwa kwa mrembo
huyo .
BABY MADAHA AENDA HEWANI
Dakika tano baada ya Madaha kufowadiwa
ujumbe huo, alikwenda hewani kwa simu
iliyomtumia ujumbe ambapo bila salamu
alisema:
“Huyo atakuwa Diamond tu, hakuna
mwingine. Mimi nimeaga kwetu , hata siku
moja Diamond asifikirie kuwa mambo yangu
yanaweza kuniendea kombo .
“Kwa chochote alichonifanyia akae akijua
lazima kimrudie hii namba nyingine kabisa,
hajui uzito wangu . Ni heri asinifuatilie ,
kitakachomtokea asubiri tu kukiona,
atajuta milele, ” alisema msanii huyo .
Alisema : “ Tatizo kubwa la Bongo, wasanii
hatupendani. Unapokwazana na mtu kidogo
tu, basi atakufanyia ubaya mambo yako
yayumbe .
“Sababu kubwa ya Diamond kuniendea kwa
‘mtaalam ’ ni lile bifu lilozuka baina yangu
na yake, ” alisema Madaha.
DIAMOND ASAKWA
Baada ya madai ya Baby Madaha, paparazi
wetu alimsaka Diamond kwa njia ya simu ili
ajibu tuhuma zinazomkabili lakini
hakupokea simu .
Ilibidi Amani limtumie ujumbe mfupi wa
maneno ( SMS) na kumweleza kila kitu ,
lakini pia supastaa huyo hakujibu kitu .
Hata hivyo , kufuatia bifu la Diamond na
Baby Madaha kumekuwa na pongezi kwenye
mitandao ya kijamii ikimpe 5 Diamond
kwamba ukimya wake wa kutojibizana na
Madaha ni ukomavu.
Wengi wamesema anachokifanya Diamond
ndiyo ustaa na si Baby Madaha ambaye kila
kukicha anaweweseka kwa jina la Diamond.
TUJIKUMBUSHE
Awali, wasanii hao waliingia kwenye bifu
zito baada ya Baby Madaha kumtupia
kashfa nzito Diamond akidai kuwa ni fuska ,
umaarufu alionao hauendani na ubora wa
kazi zake.
Katika madai hayo, Diamond alisema
hawezi kijibizana na mwanadada huyo
kutokana na ‘ levo’ yake kuwa juu .

No comments:

Post a Comment

.