Thursday, January 2, 2014

JAZBA ZATAWALA MKUTANO WA BONGO MOVIES , TRA


Na Deogratius Mongela
JAZBA baab ’kubwa imeibuka katika
mkutano wa wasanii wa filamu za Bongo
‘Bongo Movies ’ na Bongo Fleva ulioandaliwa
na Mamlaka ya Mapato Tanzania ( TRA) kwa
kushirikiana na chombo cha kusimamia haki
za wasanii nchini, Cosota .
Jacob Steven ‘JB’ .
Tukio hilo lilijiri Jumatatu iliyopita ndani ya
Ukumbi wa Vijana Social , Kinondoni , Dar
ambapo mastaa wa filamu , Jacob Steven
‘JB’ na Issa Mussa ‘ Cluod 112 ’ waliihoji
Cosota juu ya tatizo la wizi wa kazi za
wasanii ndipo ‘kiliponuka’ baada ya
kutoridhishwa na majibu.
Issa Mussa ‘Cluod 112’ .
Hali hiyo ilisababisha baadhi ya wasanii ,
wakiwemo JB na Cloud kutoka kikaoni na
kuendelea na mambo yao mengine huku
wawakilishi wa TRA wakiendelea na kikao na
kufafanua mipango yao.

1 comment:

  1. Best Real Money Casino Apps in USA 2021 - CasinoWow
    Slots Casino — One of the most recognizable online slots 1등 사이트 games around. This game's 토토 most recent is the Playtech 🏆 Best Real Money Casino App: SlotWolf🎁 #1 USA Casino Bonus: titanium ring Risk Free Spins for casinosites.one $1,000🏆 Best Real Money Casino App: deccasino SlotsMillion

    ReplyDelete

.