Thursday, January 2, 2014

MAMA KANUMBA: SIJAONA STAA WA KUMFANANISHA NA MWANANGU


MAMA wa msanii aliyekuwa nguli wa filamu
nchini marehemu Steven Kanumba , Flora
Mtegoa amenyanyua kinywa chake na
kutema cheche kuwa katika mastaa wote wa
filamu Bongo , hajaona hata mmoja wa
kumfananisha na mwanaye kimuonekano na
hata katika uigizaji wake .
Flora Mtegoa .
Akipiga stori na Centre Spread mama
Kanumba alisema hayo kutokana na mastaa
wengi kutamani awape nafasi ya kucheza
kama Kanumba katika filamu yake
anayoiandaa inayohusu maisha ya mwanaye
tangu utotoni , na kudai katika wote
hajaona mwenye kigezo cha kumpa nafasi
hiyo .
Marehemu Steven Kanumba .
“Siyo kwamba hawana kiwango kizuri cha
kumfikia mwanangu , isipokuwa kwa
mtazamo wangu naona nikimshirikisha staa
yoyote katika kipengele hicho nitakuwa
nimevurunda kazi yangu …nitaandaa
tamasha maalumu la kumsaka kijana
anayefanana na Kanumba , ” alisema mama
huyo .

No comments:

Post a Comment

.