Denis Mtima, aliyekuwa Igunga, Tabora
KWA mara ya kwanza, mzazi mwenza na
msanii wa muziki na filamu Bongo, Zuwena
Mohamed ‘Shilole’, Elias Makala ameibuka na
kujinadi hadharani wilayani Igunga, Tabora.
Shilole akiwa na mzazi mwenzake Elias
Makala.
Tukio hilo lilitokea Februari 14, mwaka huu
(Valentine’s Day) ambapo Shilole aliyekuwa
amekwenda kufanya shoo mkoani humo,
alishindwa kuzuia hisia zake baada ya mzazi
mwenzake huyo kujitokeza na kujikuta
wakioneshana mahaba mbele za watu.
Pozi hilo la kimahaba liliwashangaza watu na
kuanza kudhani kuwa huenda wawili hao
wakarudisha penzi lao lililokufa miaka mingi
iliyopita.
“Mh!
Kweli mtalaka hatongozwi, hebu ona Shilole
alivyorembua alipomuona jamaa yake, pale
Makala kumchukua ni kama kumsukuma
mlevi,” alisema shuhuda mmoja.
Shilole akiwa na mzazi mwenzake klabu.
Baada ya paparazi wetu ‘kuusoma mchezo’
huo, aliamua kumuuliza staa huyo kama
penzi lao limerudi upya au laa?
“Hahahahaa!
Kwa kweli unanichekesha kuniuliza kama
nimerudisha penzi kwa mzazi mwenzangu,
huyu ni baba wa mwanangu Joyce, itabaki
kuwa hivyo. Siwezi kumtenga na sioni ajabu
kupiga naye picha, hakuna kinachoendelea,’’
alisema Shilole.
Licha ya kufafanua hivyo, usiku wa siku
hiyo, Shilole alipokuwa jukwaani
akipagawisha mashabiki kwa shoo kali,
alimpandisha jukwaani mzazi mwenziye huyo
hali iliyozua mtafaruku mkubwa kwa mpenzi
wa sasa wa Makala aliyefahamika kwa jina la
Maguno.
Baada ya shoo kuisha, Maguno aliyekuwa na
jazba kwa mpenzi wake kupandishwa
jukwaani, alimsaka Shilole kwa udi na
uvumba kutaka kumtembezea kichapo lakini
bahati haikuwa yake, hakuweza kumpata
hadi msanii huyo aliporejea jijini Dar siku
iliyofuata.
Thursday, February 20, 2014
ALIYEZAA NA SHILOLE AIBUKA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Looh hawaendan
ReplyDeletezilipendwa hahaha!!!!! jamaa kaosha saa
ReplyDelete