Tanzania ina wanachama hai zaidi ya 600 wa
kundi la watu wenye imani ya siri ya
Freemasons wakiwa wanatokana na watu wa
kada mbalimbali wakiwemo maarufu, huku
ikielezwa kwamba miongoni mwao hakuna
viongozi wakuu wa serikali.
Hayo
yalibainishwa
na Kiongozi wa
kundi la
Freemasons
katika eneo la
Afrika
Mashariki,
Jayantilal
Keshavji Chande maarufu kama Sir Andy
Chande.
Kiongozi huyo Mtanzania mkazi wa Dar es
Salaam mwenye asili ya Kiasia, alisema licha ya
Tanzania kuwa na wanachama hao, kwa sasa
idadi ya wanachama duniani inapungua
tofauti na inavyoonekana sasa kuwa
wanaongezeka kutokana na kuibuka maneno
mengi kuhusu kundi hilo. Alisisitiza kuwa si
rahisi kumjua mwanachama wa kundi hilo, bali
wenyewe ndio wanaofahamiana, akisema ni siri
na kwamba wenyewe wanakutana katika vikao
mbalimbali mara moja kwa mwezi au zaidi.
Alisema nchini kuna wanachama zaidi ya 600
wakiwemo wafanyabiashara, watumishi
serikalini, walimu pamoja na wanataaluma
mbalimbali wanaoheshimika sana na kusisitiza
kuwa kuna maneno mengi yanayosemwa kuhusu
kundi hilo, ambayo siyo ya kweli.
Alisema idadi ya wanachama wake duniani
inazidi kupungua kutoka milioni nane hadi
sasa wako milioni sita, tofauti na wengi
wanaodhani kuwa idadi hiyo inaongezeka.
Chande alizungumza na mwandishi wa habari
hizi katika Shule ya Sekondari ya Shaaban
Robert ambako yeye ni Mwenyekiti wa Bodi ya
shule alipozungumzia maadhimisho ya miaka 50
tangu kuanzishwa kwake.
Alisema duniani kuna watu wazito wengi ambao
ni wanachama wa kundi hilo kama majaji
wakubwa na hata Binamu wa Malkia Elizabeth
wa Uingereza ni kiongozi mkubwa wa kundi hilo.
Akizungumzia masharti ya kujiunga na kundi
hilo, Chande alisema ni lazima mwanachama
huyo awe anaamini katika Mungu bila kubagua
iwapo ni Mkristo au Muislamu.
Alisema pia ni lazima anayetaka kujiunga awe
na umri unaozidi miaka 21 na walio chini ya
umri huo hawaruhusiwi kujiunga na lazima
familia ya anayetaka kujiunga na wanandugu
wafahamu kuwa umejiunga na kundi hilo.
Thursday, February 20, 2014
UKWELI HALISI...HAWA NDIO WANACHAMA WA FREEMASON TANZANIA...! SOMA ZAIDI HAPA.....
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Mmmmmmhh!!!!!! wanamwamini mungu nce kumbe sio mbaya
ReplyDelete