Tuesday, February 25, 2014

ASKOFU BILIONEA BONGO ATIKISA


ASKOFU na Nabii George David ‘Geordavie ’
wa Kanisa la Geordavie Ministry ‘ Ngurumo
ya Upako’ lililoko jijini Arusha na Kawe , Dar
hivi karibuni alifanya mkutano mkubwa na
kutikisa nchi kwa kuwa na magari ya
kifahari na ndege aina ya helikopta ‘ chopa ’
iliyokuwa ikirandaranda juu ya anga
kulinda usalama wake , Uwazi lina ushuhuda
wa kutosha .
Katika mkutano huo uliofanyika Karatu
mkoani Manyara , mwandishi wetu
alishuhudia msafara wa Geordavie ambaye
hutoa huduma ya uponyaji kwa njia za
miujiza, ukiwavutia watu wengi kwa kuwa
ulikuwa na ulinzi mkali ambao haujawahi
kutokea.
Mbali ya kuwa na chopa iliyokuwa
ikiimarisha ulinzi ambayo ameinunua hivi
karibuni , askofu huyo alikuwa na msururu
wa magari yenye thamani kubwa
yanayomfanya kutajwa kuwa tajiri kuliko
maaskofu wengine wanatoa huduma katika
makanisa ya kiroho Tanzania .
Akiwa Karatu, mbali na ulinzi binafsi,
Geordavie alikuwa akilindwa na askari wa
jeshi la polisi , askari kanzu, Askari wa
Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU ) na wale wa
usalama barabarani.
Mbali na askari hao wa serikali ambao
wamekuwa wakimlinda kila anapofanya
mikutano yake , pia Geordavie analindwa na
askari wake binafsi hali iliyowafanya
baadhi ya watu kuamini kuwa ulinzi wake ni
kama ule wa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete ‘JK ’.
“Sijawahi kumuona JK akilindwa na chopa
lakini mtumishi wa Mungu Geordavie
analindwa na ndege katika msafara wake !
Hii ni mara yangu ya kwanza kuona, ”
alisema muumini mmoja ambaye hakupenda
kutajwa gazetini .
Hata hivyo , baadhi ya watu walikuwa
wakihoji utajiri wa askofu huyo kutokana
na fedha nyingi anazozitumia anapofanya
mikutano katika sehemu mbalimbali jijini
Arusha.
“Tunajua kuwa ni tajiri , lakini anapata
wapi fedha za kutumia hivi?” alihoji
muumini aliyejitambulisha kwa jina moja la
Julius ambaye naye alihudhuria mkutano wa
askofu huyo anayetumia kaulimbiu ya
Ngurumo ya Upako katika kutoa huduma
yake.
Pia , waumini wengine walilalamikia ugumu
wanaoupata wanapotaka kumuona mtumishi
huyo wa Mungu kutokana na ulinzi mkali
anaopewa.
“Kila mtu alitamani kumuona mtumishi wa
Mungu lakini haikuwezekana kutokana na
ulinzi wake kuwa mkali, utajiri wake
hakuna mfano , hata kule nyumbani kwake
Arusha, anaishi kama Mfalme Daud , ”
alisema Fred Mushi.
Gazeti hili lilimsaka Askofu na Nabii
Geordavie kwa lengo la kutaka kujua
sababu ya kuwa na ulinzi mkali na kutumia
magari ya kifahari ikiwemo chopa katika
mikutano anayoifanya lakini simu yake
iliita bila kupokelewa.

No comments:

Post a Comment

.