KUFUATIA tukio la Ustadh Mohamed Said
Ngulangwa ( 36) , mkazi wa Mbagala -
Charambe jijini Dar kumchinja mtoto Jamal
Salum Ally ( 12) ambaye ni mwanafunzi wa
darasa la tano kisha na yeye kuuawa na
wananchi wenye hasira , Uwazi kama
kawaida yake lilichimba tukio hilo na
kubaini mengi, twende pamoja.
Mtoto Jamal Salum Ally ( 12) enzi za uhai
wake .
MTOTO AITWA , AENDA
Akizungumza na Uwazi Jumamosi iliyopita
msibani Mbagala juzi , mtoto mmoja ( jina
lipo) alisema yeye na marehemu walikuwa
wakicheza michezo ya kawaida, mara
akatokea ustadh na kumwita mtoto Jamal.
Ustadh Mohamed Said Ngulangwa ( 36 ) enzi
za uhai wake .
“Sisi tulikuwa tunacheza , ghafla ustadh
akamwita Jamal. We Jamal, njoo. Kwa vile
aliita kwa sauti ya kawaida tulijua anataka
kumtuma , Jamal akaenda mimi nikawa
namsubiria ili tuendelee kucheza , kumbe
mwenzangu aliitwa kuchinjwa , ” alisema
mtoto huyo kwa sura iliyojaa simanzi.
Waombolezaji wakiwa msibani.
KISU KIKALI CHATUMIKA
Mtoto huyo aliendelea kueleza kwa uchungu
kwamba, akiwa anamshuhudia Jamal
akikutana na ustadh , alishangaa kumwona
mwanaume huyo akimdaka kwa haraka na
kisha kutoa kisu ambapo alianza
kumchomachoma nacho na hatimaye
kumlaza chini na kukipitisha shingoni kama
anachinja kuku .
Mwili wa ustadh baada ya kuuawa na
wananchi wenye hasira kali.
“Nilipiga kelele kuwaambia watu, nikatoka
kwenda kuwaita watu huku napiga kelele
kwamba Jamal anachinjwa na ustadh , ”
alisema mtoto huyo huku akionesha sura
halisi ya masikitiko ya ndani ya moyo .
Inauma sana!
Mwili wa mtoto Jamal baada ya kuchinjwa
na ustadh .
MAJIRANI WADHANI ADHABU INATOLEWA
Nao majirani na madrasa ya mtu huyo
waliopata nafasi ya kueleza walichojua
kuhusu mauaji ya mtoto huyo , walisema
kelele za mtoto Jamal kuomba msaada
zilisikika , lakini waliamini mtoto anapewa
adhabu na mzazi wake .
MAMA WA MAREHEMU AFIKA MBIO
Maelezo zaidi yanasema kuwa , mtoto
aliyekwenda kuita watu alifika nyumbani
kwa wazazi wa marehemu na kumkuta mama
mzazi ambaye alimpa taarifa .
Eneo alilochinjiwa mtoto Jamal.
Mwanamke huyo aliyepewa taarifa hizo ,
akiwa haamini masikio yake, alitoka mbio
na kilio kuelekea eneo la tukio.
Wananchi nao baada ya kusikia maelezo ya
mtoto aliyeshuhudia , waligutuka na kutua
eneo la tukio lakini kwa bahati mbaya
walikutana na kichwa kikiwa miguuni mwa
kiwiliwili . Lazima umwage machozi !
Wananchi wakiwa eneo la tukio.
MBALI NA KIWILIWILI NA KICHWA
Wananchi hao waliweza kugundua kuwa,
kichwa hicho ni cha mtoto Jamal huku
pembeni yake kukiwa na ndoo ambayo
walidai muuaji alikusudia kukingia damu
(ili iweje ?) .
VILIO VYATAWALA , USTADH AJIFICHA
Vilio vilianza kutalawa eneo hilo, akina
mama, marafiki wa marehemu waliangua
vilio vya uchungu baada ya kuuona ukatili
huo ambao walisema haujawahi kutokea
katika eneo hilo .
Jeneza lenye mwili wa Jamal likiwa mbele ya
waombolezaji.
Ilidaiwa kwamba , wakati huo ustadh
alikuwa amejificha chumbani kwake ili
kuepuka ‘ soo ’ lake lakini wananchi
walishtukia janja yake na kutishia kuvunja
dirisha ambapo mtuhumiwa huyo
alichungulia akiwa na kisu mkononi kikiwa
na mabaki ya damudamu.
WANANCHI WAVUNJA MLANGO, DIRISHA LA
USTADH
Bila kujali kisu hicho , wananchi walivunja
mlango na dirisha na kuanza kumshambulia
kwa mawe , kisha wakamchomoa akiwa uchi
wa mnyama mpaka nje huku wakiendelea
kumshambulia hadi akakata roho.
Magari ya polisi yakiwa eneo la tukio.
BABA WA MAREHEMU NAYE ANALO NENO LA
KUSIKITISHA
Naye baba wa Jamal, Salum Ally alipoongea
na Uwazi alitoa simulizi ya majonzi, msikie :
“Nilipokea kifo cha mwanangu Jamal kwa
huzuni kubwa sana , sikuamini kama yeye
ndiye aliyeuawa kikatili namna ile!
“Nilikuwa narudi nyumbani kutoka kazini,
jirani na nyumbani nikakuta watu wengi ,
nikahoji kulikoni ? Nikaambiwa kuna mtoto
amechinjwa na aliyemchinja ameuawa .
Khaa ! Nikashangaa !
Baadhi ya watoto waliofika eneo la tukio
kushuhudia mwenzao aliyechinjwa.
“Kwa kuwa nilikuwa nimechoka sana , niliona
nifike kwangu kwanza ndipo nirudi kwenye
tukio. Kabla ya kutua kwangu, nikakutana
na mke wangu njiani huku akilia ,
nilipomhoji kuna nini , aliendelea kulia bila
kunipa majibu.
“Ndipo mpangaji mwenzangu akanipasulia
kwa kuniambia kwamba mwanangu Jamal
amechinjwa mpaka kichwa kutenganishwa
na kiwiliwili .
“Nilipatwa na mshtuko mkubwa kwani
sikufikiria kama kungetokea tukio la
kutisha kama hilo, hata kama mngekuwa
ninyi waandishi mngefanyaje jamani?
Mwili wa Jamal ukiombewa kabla ya maziko .
“Nilijivuta hadi eneo la tukio na kukuta
mwili wa mwanangu umeshafungwa kwenye
nguo na kuwekwa ndani ya gari la polisi ,
sikuwa na nguvu ya kuangalia sura yake
kwa uchungu nilioupata kwani ndiyo mtoto
wa kwanza , ” alisema Salum .
USTADAH ALIPANGA MAUAJI ?
Uchunguzi wa gazeti hili ulibaini kuwa ,
ustadh huyo alijiandaa kutekeleza mauaji
hayo kwa vile aliandaa kisu na ndoo kwa
ajili ya kukingia damu ya mtoto huyo kwa
kile watu walichodai alitaka kuinywa .
POLISI MZIGONI
Baadaye taarifa zilienea maeneo yote ya
Jiji la Dar hususan Mbagala - Charambe na
polisi walitua eneo hilo na kuchukua miili ya
marehemu wote wawili na kupelekwa chumba
cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya
Temeke.
Mwili wa Jamal ukipelekwa eneo la
makaburini kwa maziko.
Pale hospitalini, madaktari walitumia saa
mbili kichwa cha mtoto Jamal na kiwiliwili .
USTADH ATAJWA KUTOKUWA NA AKILI
Mdogo wa Ustadh Mohamed aliyekuwa
msemaji wa familia , Daudi Ngulangwa
alisema marehemu kaka yake aliwahi
kupatwa na ugonjwa wa akili mwaka
1995/ 96 kisha kupelekwa Hospitali ya Taifa
Muhimbili kutibiwa na akapona.
Maziko ya mtoto Jamal yakifanyika.
MAZISHI YAO
Marehemu Jamal alizikwa Jumamosi iliyopita
katika Makaburi ya Mbagala - Charambe
jijini Dar ( Uwazi lilikuwepo ).
Ustadh Mohamed , yeye alizikwa siku
hiyohiyo kwenye Makaburi ya Manzese jijini
Dar es Salaam.
Tuesday, February 25, 2014
USTADH ALIVYOMCHINJA MTOTO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Biblia inasema anaeua kwa upanga atakufa kwa upanga mtoto ameniuma huyo naye angechinjwa tena kimoja kimoja
ReplyDelete