Wednesday, February 12, 2014

AUNT LULU KIPIGO CHAMTULIZA

LULU Semagongo aliye mtangazaji na msanii
wa filamu Bongo, amedaiwa kupewa kipigo
cha haja na mpenzi wake aliyetajwa kwa
jina moja la Amani hivyo kujificha
nyumbani akijiuguza majeraha aliyopata .
Aunty Lulu.
Habari kutoka chanzo cha kuaminika,
zinasema kuwa Lulu alipewa kubwa na
mpenzi wake huyo mpya kutokana na tabia
zake ambazo pia hazikuelezwa.
“Nakuambia haonekani sehemu yoyote siku
hizi. Boyfriend wake mpya hana utani .
Amempiga sana , sijui alimfanya nini
mwenyewe. Huwezi kumkuta klabu wala
kwenye bendi, ” kilieleza chanzo hicho .
Gazeti hili lilimvutia waya Lulu na
kumsomea mashitaka yake, akajibu : “Nani
amewaambia hizi habari ? Hata hivyo kuna
jipya gani mtu kupigwa na mpenzi wake ? Ni
kweli nimepigwa , haya sasa mnasemaje ?
Nyie kinawauma nini ? Huyu ndiye mpenzi
wangu na nimemchagua . ”

No comments:

Post a Comment

.