MTUME na Nabii wa Kanisa la Efatha,
Joseph Elias Mwingira anayekabiliwa na kesi
ya kuzaa na mke wa mtu , hatimaye
amefunguka mengi kuhusu madai hayo
lakini amekataa kabisa kupima Ukimwi ,
Risasi Mchanganyiko lina kila kitu .
Mtume na Nabii wa Kanisa la Efatha, Joseph
Elias Mwingira .
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili katika
Mahakama ya Hakimu Mkazi - Kisutu, Dar,
umebaini kuwa Mwingira aliye na kesi
mahakamani hapo yenye namba 306 ya
2013, iliyofunguliwa na mlalamikaji Dk .
Morris William, amejibu tuhuma
zinazomkabili kwa njia ya maandishi.
Majibu hayo yameandaliwa na Kampuni ya
Uwakili ya Legal Link , ambapo nakala yake
imefikishwa kwa wakili wa mlalamikaji Dk.
William, Januari 22, mwaka huu .
Pamoja na mambo mengine , madai yaliyopo
katika jalada la kesi hiyo , mlalamikaji Dk.
William, ameomba mahakama ikubali Nabii
Mwingira apimwe Ukimwi na kipimo cha
utambuzi wa vinasaba ‘ DNA’.
Nabii huyo amepinga vikali ombi hilo ,
akieleza kuwa mahakama hiyo haina
mamlaka ya kusikiliza shauri hilo (la madai
ya kifedha ) .
MADAI YA MAPENZI
Katika majibu hayo ( nakala tunayo ) ,
Mwingira amekanusha kufanya mapenzi na
mlalamikiwa namba mbili , Dk . Phillis Nyambi
ambaye ni mke wa mlalamikaji.
“Mlalamikiwa namba moja amefafanua
kuwa hakuingia katika uhusiano wa
kimapenzi na mlalamikiwa wa pili , ”
imeeleza kampuni inayomtetea Mwingira .
AKANA KUBAKA
Nabii huyo pia amekanusha madai ya
kumbaka mlalamikiwa wa pili kama
alivyosema mlalamikaji katika hati yake ya
malalamiko iliyopo mahakamani hapo .
Nabii Mwingira pia amekana madai ya
kuzaa na mlalamikiwa namba mbili na
kuwepo kwa matatizo ya kitabibu kwa mama
huyo ambaye sasa ana mtoto mwenye umri
wa miaka mitano, akasema mlalamikaji
anatakiwa kuthibitisha.
Kuhusu madai ya Dk . Phillis kushiriki
kimapenzi na Mwingira hivyo kusaliti ndoa
halali na kumharibia furaha ya maisha
mlalamikaji, nabii huyo amesema hajawahi
kuwa na uhusiano wowote wa kimapenzi na
mwanamke huyo .
Kuhusu madai ya Mwingira kutembea na
mke wa mlalamikaji na habari hizo
kuandikwa magazetini na kwenye mitandao
ya kijamii hivyo kumdhalilisha na
kumshushia hadhi , amedai kuwa yeye
hahusiki na hilo na atahitaji kuthibitisha .
Madai mengine ya mlalamikaji kwamba
vitendo vya walalamikiwa namba moja na
namba mbili vya kujihusisha kimapenzi
vimemuathiri Dk. Morris kisaikolojia na
kiuchumi na kumfanya apoteze biashara
zake za kimataifa kwa kukosa wadhamini
katika NGO yake , Mwingira amesema kama
yametokea hakuyasababisha yeye.
Ameiomba mahakama kuitupilia mbali kesi
hiyo na kumuamuru mlalamikaji kulipa
gharama za kesi hiyo , hivyo ameweka
pingamizi la awali.
Wednesday, February 12, 2014
MWINGIRA AGOMA KUPIMA NGOMA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment