MINONG’ONO na uvumi unaotambaa kwa kasi
kuwa anajihusisha na taasisi ya wajenzi
huru ( Freemasons ) , unazidi kumtesa msanii
wa filamu za Kibongo, Mahsein Awadhi Said
‘Dk. Cheni ’ kwa madai ya kwamba anajisikia
vibaya anaponyoshewa vidole na baadhi ya
wadau wa tasnia hiyo .
Dk . Cheni .
Mwishoni mwa wiki iliyopita, mwandishi wetu
alisikia fununu kutoka kwa wadau wengi wa
filamu wakiwemo wasanii wenzake wakidai
kuwa Dk . Cheni ni mwanachama halali wa
taasisi hiyo ndiyo maana mambo yake ni
mazuri kifedha ukilinganisha na wasanii
wengine wanaoaminika kuwa na uwezo
mkubwa wa kuigiza kuliko yeye.
“Kila dalili inaonesha kabisa Dk. Cheni ni
Freemason , angalia mavazi yake mengi ni
meusi, machata na alama kibao
zinazohusishwa na taasisi hiyo , angali
fedha aliyonayo, angalia hata gari lake
lilivyojaa alama za ajabu ajabu, huyu
jamaa ni Freemason kabisa, ” alisema mdau
mmoja wa filamu ambaye hakutaka jina
lake liandikwe gazetini alipozungumza na
mwandishi wetu .
Kauli kama hizo zimekuwa zikitolewa kwa
nyakati tofauti na baadhi ya wasanii
wenzake .
Dk. Cheni alipotafutwa kwa njia ya simu
Jumapili ya wiki iliyopita na kuulizwa madai
hayo alikuwa na haya ya kusema :
“Dah ! na wewe umeyapata kaka ? Hakika
naumia sana na madai hayo, yamevuma
sana kwa wadau , tena baadhi yao ni watu
ninaowaheshimu sana , jamani mimi siyo
Freemason , naigiza , kazi zangu za u- MC
zinaniingizia kipato , najiwekea akiba .
“Si mtu wa starehe, nawekeza katika
biashara ndogondogo, madai haya ya
Freemason yananitesa sana ila namwachia
Mungu, ” alisema Dk. Cheni.
Tuesday, February 25, 2014
DK . CHENI : FREEMASON WANANITESA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment