MREMBO mmoja ambaye alihu - dumu kwenye
nyumba ya kulala wageni na baa ( jina
tunalo) iliyopo Tengeru, wilayani Arumeru ,
mkoani Arusha, Blandina Michael ( 33 )
amekutwa amekufa kwenye moja ya vyumba
vya nyumba hiyo huku chanzo cha tukio hilo
kikihusishwa na vitendo vya ushirikiana.
Taarifa za awali zilimtuhumu mmiliki wa
nyumba ya wageni moja ambaye pia
anajihusisha na biashara za madini ( jina
tunalo) kwamba alimtoa kafara mhudumu
huyo . Ilidaiwa kuwa , kila mwaka mtu
mmoja katika biashara zake hupoteza
maisha ghafla .
Hata hivyo , mfanyabiashara huyo
alipoongea na Uwazi juzikati alikanusha
vikali tuhuma hizo na kueleza kuwa yeye ni
muumini mzuri wa imani yake.
‘’Hao watu wanapotosha sana , unajua kuna
mwaka mwanaume mmoja alikufa ghafla
kwenye nyumba yangu ya kulala wageni,
alikuja na mpenzi wake ila alimeza Viagra
ambazo hata polisi walizikuta mezani .
“Sasa watu wasio na nia njema na mimi
tukio hilo wanaliunganisha na hili kwamba
nawatoa kafara , ” alisema.
Kifo cha Blandina kilitokea ndani ya
chumba huku mtu mmoja anayedaiwa kuwa
mpenzi wake aliyejulikana kwa jina moja la
Timo , mkazi wa eneo hilo akihojiwa na
polisi .
Marehemu Blandina ambaye ni mzaliwa wa
mkoa wa Tanga, anaelezwa na bosi wake
huyo kwamba alikuwa kama mtoto wa
familia yake kwa vile alimwamini sana .
Alifanya kazi hapo kwa miaka 8 na hakuwa
na tatilo la kiafya .
Bosi huyo alisema mwili wa marehemu
uligundulika baada ya mfanyakazi
mwenzake wa kiume kumpigia simu saa 2
asubuhi ambapo simu yake ilikuwa ikiita bila
kupokelewa ndipo alipoamua kwenda
kumgongea katika chumba hicho .
Alisema baada ya kufika alishangaa kukuta
mlango wa chumba chake uko wazi na
alipochungulia alibaini kwamba Blandina
alikuwa amefariki dunia.
Hata hivyo , polisi baada ya kufika na
kuufanyia uchunguzi wa awali mwili huo
hawakugundua kuwepo kwa jeraha lolote
linaloashiria kuuawa , ingawa mwili huo
ulipelekwa kufanyiwa uchunguzi wa kitaalam
katika Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru .
Jeshi la Polisi mkoani Arusha limethibitisha
kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa
mwili wa marehemu umehifadhiwa katika
chumba cha kuhifadhia maiti katika
hospitali hiyo .
Tuesday, February 25, 2014
MREMBO AFIA GESTI ARUSHA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment