Thursday, February 20, 2014

Facebook yasema itainunua WhatsApp


Facebook na WhatsApp ni maarufu sana
miongoni mwa vijana.
Kampuni ya mtandao wa Kijamii ya Facebook
imesema kuwa itanunua mtandao wa
mawasiliano ya ujumbe mfupi wa WhatsApp kwa
kima cha dola bilioni kumi na sita, na nyongeza
zaidi ya dola bilioni tatu zitakazolipwa
waanzilishi wa mtandao huo pamoja na
wafanyikazi wake.
Hiyo ndiyo biashara kubwa zaidi ya ununuzi
kuwahi kutekelezwa na Facebook hadi kufikia
sasa.
WhatsApp ni maarufu sana miongoni mwa
vijana wanaotafuta kuepuka kulipia huduma ya
kutuma ujumbe mfupi wa simu yaani SMS.
WhatsAp imeweza kuwasajili zaidi ya watumiaji
milioni mia nne hamsini.
Katika taarifa, mwanzilishi wa Facebook Mark
Zuckerberg amesema kuwa mtandao huo upo
njiani kuwaunganisha watu bilioni moja jambo
litafanya Facebook kuwa na thamani kubwa.

2 comments:

  1. jambo la msingi sna myb tutapata kitu kipya maana fb kma hawana kitu kpya vile

    ReplyDelete
  2. whatsapp ninoma fb wenyewe wanasanda ndio maana wameamua kuinunua

    ReplyDelete

.