Thursday, February 20, 2014

VAZI HILI LA DIAMOND LASABABISHA VIDEO YA MSANII DULLY SYKES KUFUNGIWA


jana Prince Dully Sykes akiongelea kufungiwa
kwa video yake ya kabinti special na Baraza la
Sanaa Tanzania(BASATA) . Kuna sababu kuu
mbili zilizosababisha video hii kufungiwa na ya
kwanza ni kitendo cha msanii Diamond
Platnumz kuvaa T-shirt iliyoandikwa neno
ambalo ni tusi . Hii ingekua kwa nchi za mbele
basi ungekutwa t-shirt hii wanaifanyia kitu
kinaitwa “blurring” yaani wanayafanya
maneno yasisomeke lakini wabongo wakaona
isiwe tabu na director akaamua kuacha video
irushwe ikiwa katika hali hii.
Sababu ya pili ni vazi la ufukwe yule demu
alilovaa kitu ambacho dully ameona haikua
mbaya.
Je, Unadhani ni haki video hii kufungiwa na
kama ni haki je unafikiri ifungiwe ni
kwasababu ipi ya msingi?

2 comments:

  1. BASATA wamechelewa waache tu domondi kazingua sio maneno poa kuiga maghalibi akujengi

    ReplyDelete

.