Wednesday, February 12, 2014

INSTAGRAM KIMENUKA ASEE!BAADA YA KAJALA KUDAIWA ANATEMBEA NA CLEMENT WA WEMA

Huko instagram hali si shwari tena!baada ya kuibuka mtubmwenye account yenye jina la @kajala55 na kuanza kumshutumu kajala kuwa sio rafiki wa kweli kwa Wema sababu anatembea na aliyekuwa mpenzi wa Wema yaani Clement akaendelea kudai kuwa huyo clement kanunulia kajala gari na mazagazaga mengine..akaendelea kutiririka kuwa Kajala si mtu mzuri kabisa kwani mpaka masaloon anapoenda huwa anamsema wema kuwa mjinga na mpumbavu sababu amechezea shilingi chooni kipindi yupo na clement.Baada ya huyu @kaja55 kutiririka Wema nae aliweka post kuthibitisha kuwa kajala ni best friend wake na hakuna kitakachowatenganisha!na huo ni uongo mtupu sababu kila achofanya kajala wema anajua kila kitu so hakuna kitu kama hicho,huku kasheshe hilo likiendelea Teamwema wanahisi hiyo account ya kajala55 ni ya team penny ambao wameshindwa kumzingua wema sasa wameamua kumzingua kajala huku wakijua itamjusa wema, msanii batulia aliingilia kati kwa kuwaambia kama hizo habari ni za kweli waweke ushahidi japo kidogo ndio watu waamini ,mpaka tunaingia mitamboni hakukua na dalili zozote za wao kuhahidi kutoa ushahidi wa madai hayo.

Imeandikwa na ®Team Wakishuaz Blog kwa hisani ya INSTAGRAM

1 comment:

.