Thursday, February 27, 2014

KAJALA MASANJA ANYWESHWA SUMU


Staa wa sinema za Kibongo, Kajala
Masanja.
Stori : Shakoor Jongo
STAA wa sinema za Kibongo, Kajala
Masanja amejikuta katika hali mbaya
kufuatia kunyweshwa sumu na mtu ambaye
hakuweza kufahamika mara moja .
Tukio hilo lilitokea usiku wa Jumapili
iliyopita maeneo ya Tegeta jijini Dar katika
Klabu ya Seventy One ambayo alikwenda
kujiachia na marafiki zake.
Chanzo cha uhakika , kilipenyeza habari
kuwa, Kajala alinyweshwa sumu hiyo kupitia
kwenye glasi ambayo aliwekewa juisi ambapo
haikuweza kufahamika mara moja kuwa
aliwekewa kabla au baada ya mhudumu
kumpa huduma .
“Unajua mambo ya klabu tena , kila mtu
alikuwa bize na mambo yake , hivyo
hatukuweza kugundua mara moja kuwa
nani alihusika, lakini tulishangaa ghafla
Kajala alijisikia vibaya hivyo marafiki zake
wa karibu walimkimbiza nyumbani kwao
kisha hospitali, ” kilisema chanzo hicho .
Baada ya paparazi wetu kuzinyaka habari
hizo , Jumanne iliyopita (juzi ) alimtafuta
Kajala ambaye alikuwa amejipumzisha
nyumbani kwa njia ya simu , akaeleza kwa
shindashinda jinsi tukio hilo lilivyokuwa:
“Ilikuwa Jumapili usiku , nilikuwa nimekaa
na washkaji zangu pale klabu akiwemo
Mubenga, sasa niliagiza juisi pale nikaanza
kunywa, funda la kwanza … la pili nikaanza
kujisikia vibaya.
“Nilisikia kama kichefuchefu , nikatoka nje
ambapo hali ilizidi kuwa mbaya . Marafiki
wakashauri nirudishwe nyumbani, nako hali
ikazidi kuwa mbaya .
“Wakanipeleka hospitali ambapo madaktari
waliponipima walinambia nimekunywa kitu
chenye sumu hivyo wakanipa dawa za
kuondoa sumu mwilini na nashukuru Mungu,
naendelea vizuri.”
Alipoulizwa kama ana ufahamu wowote juu
ya aliyehusika na kama anaweza
kumchukulia hatua zozote , Kajala alisema
anamuachia Mungu kwani anaendelea
vizuri.
“Mimi nashukuru bado napumua , siwezi
kujua aliyefanya hivyo alikuwa na dhumuni
baya kwangu au iliingia kwa bahati mbaya ,
naendelea vizuri, ” alisema.

No comments:

Post a Comment

.