Thursday, February 27, 2014

EE! MUNGU : MFANYABIASHARA WA MAGARI ANASWA AKITAKA KUMLAWITI MODO MAARUFU


Stori : Waandishi Wetu
EEH Mungu! Unaweza kukataa lakini ni
ukweli kwamba dunia imekwisha ! Mambo
yanayotendeka kila kukicha juu ya ardhi
yanathibitisha hilo.
ANGALIA VIDEO HII JINSI KAMANDA WA OFM
ALIVYOFANIKISHA TUKIO HILI KUPITIA
GLOBAL TV ONLINE
OFM walivyomnasa mfanyabiashara wa
magari (kushoto ) chumbani akitaka
kumlawiti modo maarufu .
Mfanyabiashara maarufu wa magari jijini
Dar es Salaam aliyefahamika kwa jina la
Juvenali amekumbwa na aibu ya mwaka
baada ya kunaswa mtupu chumbani na
mmoja wa wabunifu wa mavazi ‘modo ’
maarufu Bongo ( jina tunalihifadhi kwa
sasa kwa sababu za kimaadili).
. ..amefungwa pingu .
Tukio hilo la aibu lilimkuta mfanyabiashara
huyo nyumbani kwake, Mbezi ya Tangi - Bovu
jijini Dar es Salaam hivi karibuni ambapo
wawili hao walinaswa chumbani wakiwa
watupu katika mtego maalum.
KISA KILIPOANZIA
Chanzo cha kufichuka kwa taarifa hizo ni
modo huyo kumwonesha kaka yake (naye
jina tunalo) meseji ‘tamutamu ’ kutoka kwa
mfanyabiashara huyo kwenda kwake
akimshawishi kumlawiti.
KAKA MTU ACHARUKA
Ilidaiwa kuwa kaka mtu alikasirika,
aliamini kitendo cha mfanyabiashara huyo
kutaka kumlawiti mdogo wake ni
kuidhalilisha familia .
“Kaka akamwambia mdogo wake kwamba ni
lazima wamtege jamaa huyo ili kumshikisha
adabu na ache tabia hiyo , ” kilisema chanzo.
na Polisi .
KAKA ACHUKUA GAZETI , APIGA SIMU OFM
Baada ya kukubaliana na mdogo wake ,
kaka huyo alitafuta Gazeti la Amani na
kukutana na namba za Kamanda wa
Oparesheni Fichua Maovu ‘ OFM ’ na kuzipiga .
Kaka : Jamani poleni na kazi , hapo ni OFM ?
OFM: Tumepoa ndugu , ndiyo sisi , tena
unaongea na mimi kamanda mwenyewe.
Niambie ndugu yangu , bila shaka unataka
kutupatia kazi , tupo tayari .
Kaka : Ni kweli , kuna jamaa mmoja ni
mfanyabiashara wa magari , anamtumia
meseji mdogo wangu akimshawishi amlawiti .
Tukio hili limenikera sana . Naomba tukutane
ili tupange jinsi ya kumnasa ili kukomesha
tabia hii .
Nimeshazungumza na mdogo wangu na yupo
tayari kwa jambo hilo ili tumtege,
tukamilishe hiyo kazi kukomesha huu
upuuzi.
OFM: Sawa kabisa, inawezekana .
Kilichoendelea hapo ilikuwa ni OFM kumpa
baadhi ya maelekezo kaka mtu,
wakakubaliana kila kitu namna mchezo
ambavyo ungekamilika kwa mbinu za
kitaalam za makachero wa OFM.
... Mfanyabias
huyo akichukuliwa na polisi .
OFM YAPOKEA KAZI , YARIPOTI POLISI
Baada ya kukutana na kaka wa modo huyo
na kupanga kila kitu , OFM iliwasiliana na
Jeshi la Polisi Kituo cha Mbezi - Makonde,
Dar ambapo taarifa za uovu huo zilikuwa na
dalili ya kufanyika karibu na maeneo hayo.
Mkuu wa kituo hicho alitoa ‘ vijana ’ wake
wawili, shupavu waliojitambulisha kwa
majina ya Afande Nassoro na Afande Sele.
Wakakamavu kabisa.
... Safari ya
kuelekea kituo cha polisi cha Kawe.
KATIKA ENEO LA TUKIO
Fasta, OFM na askari hao walielekea Mbezi
Tangi - Bovu , kituo cha daladala eneo la
mtego ambapo mfanyabiashara huyo
alimuahidi kijana huyo akamchukulie hapo
kwenda naye kwenye nyumba ya kumfanyia
usodoma.
MFANYABIASHARA AFIKA NA GARI
Wakiwa mita kadhaa , OFM na polisi ,
walimuona mfanyabiashara huyo akiwasili
na gari aina ya GX 100 ( namba za usajili
tunazo ). Alifunga breki miguuni kwa kijana
huyo , akamfungulia mlango , naye akazama
ndani .
Safari ilianza kuelekea upande wa
Bagamoyo lakini mita chache gari hilo
lilikata kulia . OFM na maafande walikuwa
wakifuatilia kwa nyuma bila kujulikana .
kituo cha polisi .
GARI LAFIKA NYUMBA YA TUKIO
Baada ya mwendo wa kama kilometa mbili,
gari hilo lilifika kwenye nyumba moja na
kupiga honi kisha geti likafunguliwa , gari
likaingia na geti likafungwa.
MODO NDANI YA CHUMBA CHA TUKIO
OFM, maafande wakiwa nje , wawili hao
tayari walikuwa chumbani ambapo dogo
huyo aliwasiliana na ‘ makachero ’ wa nje na
kuwaambia kwamba mfanyabiashara huyo
alishasaula nguo na yupo kama
alivyozaliwa , alikuwa katika hatua za awali
za kutaka kukamilisha ufirauni wake . Hapo
sasa OFM na polisi wakajipanga kuchoma
ndani kuzuia unyambisi huo.
KIZINGITI
Hata hivyo , OFM na askari hao walishindwa
kuingia baada ya geti kufungwa kwa ndani
na aliyefunga kutoka nje kwa kutumia
mlango mwingine .
Hata hivyo , askari walitumika ukomandoo ,
‘timu ’ ikafanikiwa kuzama ndani moja kwa
moja na kwenda kugonga katika chumba
husika ( wale askari hatari sana aiseee!).
AFUNGUA MLANGO BILA WASIWASI
Bila kujua kuwa OFM na polisi ndiyo
waliogonga mlango , jamaa huyo alifungua
mlango na kukutwa akiwa mtupu sanjari na
modo huyo .
SHETANI ATUPIWA ZIGO
Maafande walimuuliza ‘ biznesmani’ huyo ni
kwa nini wamekutwa uchi tena wanaume
watupu chumbani , alijibu kuwa walikuwa
wanahisi joto ndiyo maana waliamua kuvua
nguo zote .
Lakini akaongeza: “ Jamani niacheni. Hii ni
aibu , nitawapeni chochote kile mnachotaka,
shetani ndiye alinipitia jamani.”
SAFARI KUELEKEA LUPANGO
Mfanyabiashara huyo alichukuliwa na
askari hao hadi polisi lakini baadaye
akahamishiwa Kituo cha Kawe ambako
shauri hilo liliandikishwa na kupewa jalada
la kesi namba KW/ RB/ 1747/ 2014.
Baada ya kuchukuliwa maelezo ,
mfanyabiashara huyo aliswekwa lupango
akisubiri sheria kuchukua mkondo wake .
OFM
OFM kama ilivyotambulishwa awali, ipo kwa
ajili yako wewe Mtanzania unayeona uovu
katika jamii na vyombo husika vikashindwa
kuchukua hatua, kwa OFM kila kitu
kinawezekana ! Wanaweza kuingia popote na
kuchunguza uovu wowote kwa mafanikio
makubwa – tuletee kazi tutaifanya .

No comments:

Post a Comment

.